WITO UMETOLEWA KWA WAMILIKI WA VIWANDA KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA WADADISI WANAOKUSANYA TAARIFA ZA SENSA YA VIWANDA NCHINI.

Waziri
wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mkoani Dodoma kuhusu maendeleo
ya zoezi la Sensa ya Viwanda linalofanyika nchini. Kushoto kwake ni Idd
Mruke, Meneja Takwimu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, mkoa wa Dodoma.

Meneja
wa Takwimu za Biashara na Utalii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu,
ambaye ni Msimamizi wa Sensa ya Viwanda nchini akiwaelezea waandishi wa
habari leo mkoani Dodoma kuhusu vigezo vilivyotumika katika kuchagua
sampuli ya viwanda vilivyochaguliwa kufanyiwa utafiti. Kushoto kwake ni
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda.

Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Viwanda na
Biashara Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda wakati akizungumza nao leo mkoani
Dodoma kuhusu maendeleo ya zoezi la Sensa ya Viwanda linalofanyika
nchini.
No comments:
Post a Comment