MSAFARA WA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA WAWASILI WILAYANI KAHAMA USIKU HUU KWA BASI,KESHO KUANZA RASMI ZIARA YA KAGERA

KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa
na kamati ya Ulinzi na Usalama usiku huu ndani ya wilaya Kahama mkoani
Shinyanga tayari kwa mapumziko,ambapo kesho ataianza rasmi ziara yake
katika kijiji cha Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera,Ndugu
Kinana ndani ya Biharamulo atapokea taarifa za chama na Serikali na
baadae kuzungumza na Wafugaji wa kanda ya Ziwa (Mikoa ya
Geita,Kagera,Mwanza na Shinyanga) na baadae kueleke Bukoba mjini.
Ndugu Kinana amewasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua
utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha uhai
wa chama,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama.

KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akipokelewa na
Mbunge wa jimbo la Nzega usiku huu Dkt.Hamis Kingwangalla,mara baada ya
kuwasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika
ziara yake ya kikazi ya kukagua
utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha
chama.Ndugu Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama.

KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akipokelewa na
baadhi ya viongozi wa chama hicho usiku huu wilayani Nzega mkoani Tabora
akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua
utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha
chama.Ndugu Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama.

KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akiwa na baadhi
ya viongozi wa chama na serikali mara baada ya kuwasili wilayani humo
akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua
utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha
chama.Ndugu Kinana pia aliwashukuru wakazi wa wilaya hiyo kwa kumpokea
vyema na kumtakia kheri katika safari yake ya kujenga chama na nchi kwa
ujumla

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akiwashukuru wapenzi na washabiki wa chama hicho wilayani
Nzega usiku huu kwa kumpokea vyema na kumtakia kheri katika safari yake
ya kukijenga na kukiimarisha chama na nchi kwa ujumla

KATIBU
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akimshukuru
Mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kingwangalla kwa mapokezi mazuri wilayani
humo,ndugu Kinana amewasili wilayani humo mnamo majira saa nne usiku na
ushehe akitokea jijini Dar kwa basi maalum akiwa emeambatana na ujumbe
wake akielekea mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi

Mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kingwangalla akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana .
PICHA NA MICHUZI JR.KAHAMA.
No comments:
Post a Comment