KATIBU MKUU WA CCM KINANA AANZA ZIARA MKOANI KAGERA LEO, AKUTANA NA MAKUNDI YA WAFUGAJI KANDA YA ZIWA.

Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa mapema leo katika uwanja wa shule
ya msingi Nyakanazi,Wilayani Biharamulo mkoani Kagera,ambapo pia
aliwasalimia wananchi wa kijiji hicho tayari kwa kuanza ziara rasmi
mkoni humo.Kinana yupo Mkoani humu kwa ziara ya kikazi ya siku kumi ya
Kukagua utelekezwaji wa Ilani ya chama cha CCM ya mwaka 2010 pamoja na
kuimarisha chama na kusikiliza matatizo ya wananchi.

Kinana akisalimiana baadhi ya Wananchi wa Nyakanazi mapema leo,alipopita kuwasalimia.


katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa ameambatana Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye (aliyebeba mtoto),wakiwasalimia wananchi wa kijiji
cha Nyakanazi,wilayani Biharamulo mkoani Kagera

Wananchi
wa kijiji cha Nyakanazi pamoja na wapenzi/washabiki wa chama cha CCM
wakishangilia kwa ujio wa Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Ndugu Kinana mkoani
Kagera.

Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwasalimia Wananchi wa kijiji cha Nyakanazi
pamoja na wapenzi/washabiki wa chama cha CCM waliofika kumsikiliza
mapema leo asubuhi,mkoani humo.Ndugu Kinana akiwa ameambatana na Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya maofisa wa chama hicho
wako ziarani kanda ya ziwa kwa siku 28 za Kukagua utelekezwaji wa
Ilani ya chama cha CCM ya mwaka 2010 pamoja na kuimarisha chama na
kusikiliza matatizo ya wananchi.

Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye na wafuasi wa chama hicho wakikatiza kuelekea kwenye mkutano wa
ndani na pia kuzungumza na kundi la Wafugaji


Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na ujumbe wake akikatika kwenye moja ya soko
katika kijiji cha Nyakanazi,Wilayani Buharamulo mkoani Kagera mapema leo
asubuhi,akielekea kwenye mkutano wa kupokea taarifa za Chama na
serikali pamoja na kuyasikiliza makundi ya Wafugaji kuhusiana na
matatizo waliyonayo.
No comments:
Post a Comment