KINANA AITAKA SERIKALI KURAHISISHA UTOAJI WA LESENI KWA WAFANYABIASHARA,MADEREVA WA MAGARI NA BODABODA

Wananchi wa Ngara mjini wakishangilia jambo katika mkutano wa hadhara wa CCM

KATIBU
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa mji wa
Ngara Mjini kwenye mkutano wa hadara,Nape Nnauye alisema kuwa hakuna
sababu ya Watanzania kuingia kwenye mpasuko kwa sababu ya mchakato wa
katiba mpya na kuashauri ni vema mjadala ukafungwa kwenye nyumba za
ibada. Amesema inasikitisha unapoona baadhi ya viongozi wa dini badala
ya kuhubiri neno la Mungu na kuwaunganisha Watanzania wanatumia nafasi
yao kuwagawa wananchi kwa sabababu ya Katiba mpya.

KATIBU Mkuu wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM), Abdulrhaman Kinana akiwahutubia wananchi wa Ngara mjini,Kinana ameitaka Serikali kurahisisha utoaji wa
leseni kwa wafanyabiashara , madereva wa magari na bodaboda badala ya kuacha
watu wanasumbuka kutafuta leseni umbali mrefu tena kwa gharama kubwa.
Kinana amesema kuwa moja ya
ombi la wananchi hao ilikuwa ni kuomba kurahisishiwa kupata leseni ili kuondoa
usumbufu wanaoupata sasa.Alisema Serikali lazima
iweke mazingira mazuri ya kutoa leseni kwa wananchi wakiwamo wafanyabishara na
madereva bodaboda huku akieleza hakuna sababu ya kutumia gharama kubwa kwa
ajili ya leseni.

Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Chanjo ya watoto
kuzuia maambukizi ya magonjwa katika kata ya Nyakisasa kijiji cha
Kashinga akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ngara mkoani
Kagera,lengo la ziara hiyo likiwani ni kukagua utekelezaji wa ilani ya
Uchaguzi ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa chama, Katika ziara hiyo
Kinana anaongozana na ktibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na
viongozi mbalimbali wa CCM kutoka mkoa wa Kagera.

Baadhi ya akina mama na watoto wao wakisubiri watoto wao kupatiwa chanjo katika zahanati ya kijiji cha Kashinga wilayani Ngara.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi hawapo
pichani wakati alipozindua chanjo ya watoto katika zahanati ya Kashinga
akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Ngara leo wa tatu kutoka kulia ni
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM na katikati ni Mkuu wa
mkoa wa Kagera Mh. John Mongella

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu katika zahanati hiyo. 

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wa CCM wilayani Ngara
wakishiriki kwa pamoja katika ujenzi wa ofisi ya CCM tawi la Munjebwe,
Rulenge.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Rulenge.

Baadhi
ya Wafuasi wa chama cha CHADEMa wakikabidhi kadi zao kwa Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Kinana,na kutangaza kujiunga na chama chama CCM.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi mbalimbali za
waliokuwa wanachama wa Chama cha CHADEMA mara baada ya kurejesha kwake
na kujiunga na CCM katika mji wa Rulenge.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ngara Mama Constansia Buhie wakizikusanya
kadi mbalimbali za wafuasi wa upinzani na kuzikabidhi kwa viongozi hao
wa CCM,ikiwa ni ishara ya kujiunga na chama hicho cha CCM

Baadhi ya kadi zilizorejeshwa kwa Kinana na wananchi hao na kujiunga na CCM.

Kwaya
ya akina mama wa Rulenge wakiimba wimbo maalum wakati wa mkutano wa
hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mzee Godwin Magambo wakati alipowasilisha malalamiko yake ya ardhi

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mhandisi wa kampuni
ya kichina ya TKPE Bw.Ton Minyang wakati alipokagua ujenzi wa Mtambo
wa umeme vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa kata ya
Kabanga wilayani Ngara.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua kkikundi cha akina mama
wajasiriamali cha mjini Ngara kabla ya kuhutubia mkutano wake na
wananchi mjini humo leo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata keki kuashiria uzinduzi wa kikundi hicho cha akina mama wajasiriamali.
No comments:
Post a Comment