HUAWEI TANZANIA NA WIZARA YA MAWASILIANO,SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUUNGANA KATIKA KONGAMANO LA TEKNOHAMA NCHINI
Mkurugenzi
wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally
Simba Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam jana kuhusu
kuungana na kampuni ya Huawei katika kongamano la Teknohama, kulia ni
Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa Huawei Tanzania Samson Majwala.
Mkurugenzi
wa masoko na mauzo wa Huawei Tanzania Samson Majwala kiongea na
waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam jana kuhusu kuungana na Wizara
ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia katika kongamano la Teknohama
kushoto ni Mkurugenzi wa ICT katika wizara ya mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia Dk Ally Simba
Mkurugenzi
wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Dk Ally
Simba (Kushoto) wakishikana mkono na Mkurugenzi wa masoko na mauzo wa
Huawei Tanzania Samson Majwala kuashilia kuungana katika kongamano la
Teknohama.
Kampuni
ya Huawei Tanzania ikishirikiana na Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na
Technolojia jana ilitangaza kuwepo kwa kongamano la kwanza la Huawei
Cloud Conference katika ukumbi wa Julius Nyerere Convential Center JNICC
tarehe 18 na 19 Juni 2015.
Kongamano
hilo litajadili hali ya sekta ya tecknohama kwa sasa,sera mpya
zitakazowekwa na kuweka ajenda ya jinsi ya kukuza sekta hiyo nchini.pia
kongamano hilo litaainisha jinsi nchi itafikia malengo yake ya milenia
kupitia tecknohama.
Mkurugenzi
wa ICT katika Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Dk. Ally
Simba alisema, “tumefurahi sana kwamba Wizara na kampuni ya Huawei
Tanzania zitashirikiana katika kongamano hilo,ambapo tutajadiliana kwa
undani ukuaji na maendeleo katika sekta ya ICT.Na kwa upande wa Wizara
tutaelezea sera mpya na mipango tulioweka ili kuhakikisha maendeleo ya
sekta”.
Aliendelea
kwa kuwahakikishia Watanzania kwamba Wizara imejikita katika kukuza
sekta ya Teknohama.aliongeza kwamba Makamo wa Rais wa jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania anategemewa kuwa mgeni rasmi,huku pia ,Waziri na
Katibu Mkuu wa Wizaraya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia na Balozi wa
China nchini Tanzania watakuwepo.
Kwa
upande wake,Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Huawei Tanzania, Bwana
Samson Majwala alisema, “tunaishukuru sana Wizara kwa kukubali kuungana
nasi katika kuandaa kongamano la kwanza la Huawei Cloud Conference
nchini Tanzania,na tunawahakikishia Watanzania wote kwamba kongamano
litapendeza.
Tutakua na wataalam kutoka nyanja tofauti za Teknohama kutoka serikalini na kampuni ya Huawei ambao watatuelimisha kuhusu mitindo mipya katika sekta hiyo.Sisi kama Huawei tutaelezea mipango tuliyonayo ya kuboresha sekta hii nnchini Tanzania”.
Tutakua na wataalam kutoka nyanja tofauti za Teknohama kutoka serikalini na kampuni ya Huawei ambao watatuelimisha kuhusu mitindo mipya katika sekta hiyo.Sisi kama Huawei tutaelezea mipango tuliyonayo ya kuboresha sekta hii nnchini Tanzania”.
Katika
kongamano hilo,Huawei watazindua bidhaa zao mpya za Oceanstor V3 na
Fusonq.Pia kutakua na gari maalumu la kufanya maonesho,gari hilo kwa
kila mwaka linafanya ziara katika mabara yote duniani,na kwa mwaka wa
2015 litazuru bara la Afrika haswa Afrika kusini na Afrika
Mashariki,Tanzania ikiwemo ya nchi itakayopita.
No comments:
Post a Comment