HOTUBA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA (Mb) KWENYE MKUTANO WAKUTANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS

Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward
Lowassa ahutubia wananchi kwenye Mkutano wa hadhara, wakati akitangaza
nia yake ya kuwania Urais wa Awamu wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia tiketi ya CCM.
--------
HOTUBA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA
(Mb) KWENYE MKUTANO WA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA KUPITIA CCM
UTANGULIZI:
Ndugu viongozi, wana-CCM na Watanzania
wenzangu; Kwanza nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetufikisha hapa
leo. Lakini pia niwashukuru nyote mlioweza kufika hapa leo. Kipekee
niwashukuru CCM wenzangu na Watanzania kiujumla ambao wameendelea kuwa
marafiki na kuniuunga mkono.…

Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward
Lowassa ahutubia wananchi kwenye Mkutano wa hadhara, wakati akitangaza
nia yake ya kuwania Urais wa Awamu wa tano wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia tiketi ya CCM.
--------
HOTUBA YA MHESHIMIWA EDWARD LOWASSA
(Mb) KWENYE MKUTANO WA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA KUPITIA CCM
UTANGULIZI:
Ndugu viongozi, wana-CCM na Watanzania
wenzangu; Kwanza nianze kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetufikisha hapa
leo. Lakini pia niwashukuru nyote mlioweza kufika hapa leo. Kipekee
niwashukuru CCM wenzangu na Watanzania kiujumla ambao wameendelea kuwa
marafiki na kuniuunga mkono. Hakika nimejawa na furaha.
Hii ni siku muhimu kwangu na kwa nchi yetu.
Leo nimeamua kuwaita ili kuwatangazia rasmi azma yangu ya kuomba ridhaa
ya chama chetu, Chama Cha Mapinduzi (CCM), ili niteuliwe kukiwakilisha
cha chetu kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Naamini historia itaihifadhi kama ni siku
ambayo kwa mara ya pili katika maisha yangu, nimejitokeza kuwania
kuiongoza nchi yetu kupitia chama chetu. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka
1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi hapa nchini
nilipojitokeza nikiwa pamoja na Rais Jakaya Kikwete;
Wakati ule sote tulikuwa wanasiasa vijana.
Pamoja tulikwenda kuchukua fomu na baadaye kwa pamoja tukazungumza na
waandishi wa habari. Tulileta hamasa kubwa pale tulipofanya jambo ambalo
halikuzoeleka kwa Watanzania kwa kutangaza kwamba yeyote atakayepita
kati yetu, mwenzake ambaye hatafanikiwa angemuunga mkono.
Ningeweza kujitokeza tena mwaka 2005 lakini nikaamua kwa dhati kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete.
Nikiwa Mwenyekiti wa Kampeni niliwaongoza
wenzangu kufanikisha ushindi mkubwa wa mgombea wetu, na baadaye ushindi
mkubwa wa asilimia 80 kwa Chama Cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa
2005.
Nitaeleza kwa nini nimeamua kujitokeza
tena, na kwa nini naamini mimi ndiye mtu sahihi wa kuiongoza nchi yetu
wakati huu. Mpaka hapa itoshe tu kuwaeleza ni kwa nini naamini leo ni
siku muhimu. Ni siku muhimu kwa sababu nina kiu ya kuona Watanzania
wenzangu tunajiunga kuianza safari ya matumaini.
Ni siku muhimu kwa nchi yetu pia, kwa
sababu naamini inajibu wito wa mahitaji ya sasa ya uongozi wa Taifa letu
wa kumpata kiongozi imara atakayewaongoza Watanzania kujenga taifa
imara. Na hili nitalieleza kwa kina. Hii ndiyo safari ya matumaini.
CLICK HAPA KU-DOWNLOAD HOTUBA KAMILI===>
No comments:
Post a Comment