HISPANIA YASAIDIA BILIONI 3.1/- KUKABILI UMASKINI TANZANIA
Balozi
wa Spain nchini, Mh. Luis Cuesta Civis (kulia) na Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) wakiwasili kwenye
ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo kabla ya ziara ya kuelekea
katika kijiji cha Chasimba kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF
katika wilaya ya Bagamoyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Ladislaus Mwamanga.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Modewjiblog team, Bagamoyo.
SERIKALI
ya Hispania imetoa shilingi bilioni 3.1 kusaidia miradi ya maendeleo ya
jamii nchini ambayo mingine inatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya
Jamii, TASAF.
Fedha
hizo zimetolewa kupitia mfuko wa maendeleo endelevu (SDGF) zilizotolewa
kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya shughuli zake hapa
nchini. Mashirika
hayo ni Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ,Shirika la
Umoja wa Mataifa la watoto (UNICEF) , Shirika la Umoja wa Mataifa la
Idadi ya watu (UNFPA), na Shirika la Kazi Duniani( ILO).
Hayo
yamesemwa katika ziara ya Balozi wa Hispania nchini, Luis Cuesta Civis
na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez
katika kijiji cha Chasimba kilichopo wilayani Bagamoyo, Pwani jana.
Ziara
yao ilikuwa ya kukagua miradi inayofadhiliwa na TASAF katika wilaya ya
Bagamoyo. Bagamoyo ni miongoni mwa wilaya nane zilianza kupokea fedha za
TASAF na kuonekana kuleta mabadiliko makubwa katika jamii. Hata hivyo moja ya shughuli wanazofanya wakazi wa Chasimba ni kilimo wakiwa na pato la sh 350,000 kwa mwaka. Huduma za jamii zinazopatikana katika vijiji hivyo ni pamoja na shule ya msingi, barabara inayopita kijiji ni hapo na zahanati.
Wakati
wa utekelezaji wa awamu ya pili ya TASAF jamii ya Chasimba ilijenga
madarasa matatu na ofisi ya walimu. Miradi hiyo ilizinduliwa mwaka 2007
na kukamilika mwaka 2008. Katika miradi hiyo TASAF ilichangia
30,415,471.
No comments:
Post a Comment