WANAFUNZI UDOM WAGOMA WAKIDAI PESA ZAO ZA MIKOPO KWA AJILI YA KUJIKIMU







WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha UDOMA, Mkoani Dodoma wameamua kuacha
masomoyao tangu jana na kugoma wakishinikiza Bodi ya Mikopo kulipa pesa
zao za mikopo kwa ajili ya kujikimu.
Mgomo huo unakuja siku mbili tu baada ya wenzao wa UDSM, Dar es
Salaam kugoma kwa madai kama hayo na hatimaye siku iliyofuatia wakalipwa
pesa zao.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alilazimika kumtuma Naibu Waziri wa Afya
Steven Kebwe na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa ili kuwatuliza
wanafunzi hao waliokuwa wakidai kuishi katika mazingira magumu baada ya
kukoswa pesa za kujikimu na kufanya kushindwa kufuatilia masomo yao.
Hali hiyo ilionekana kama kutulia kwa muda, lakini leo yameibuka
mapya baada ya wanafunzi haokugoma tena wakiendelea kudai pesa zao za
mkopo.
Akizungumza na mwandishi wetu, mwanafunzi mmoja wa UDOM (kwa sharti
la kutotajwa jina lake kutajwa) alisema kuwa, "asubuhi ya leo tumegoma
kuingia madarasani tukidai haki yetu, pesa zetu za mkopo hatujapata,
tunaishi katika mazingira magumu. Maisha ya hapa chuo yamekuwa magumu
sana, kwa mfano mimi nimekopa pesa kama laki moja mpaka sasa tangu hali
hii ya kukoswa 'boom' ianze lakini bado maisha yamekuwa magumu kwa
upande wetu. Tunalazimika kula mara moja kwa siku. Tunaomba serikali
isikilize kilio chetu tunapata shida sana, tuanshindwa kufuatilia masomo
yetu kwa kutumia muda mwingi kuwaza tutakula nini, tutaishi vipi na
mpaka lini kwa hii hali."
Taarifa zinaongeza pia kuwa wamepigwa mabomu ya machozi na Jeshi la
Polisi likiwataka kutawanyiaka eneo walilokuwa wamekusanyika. Kikosi cha
kuzuia ghasia maarufu kama FFU wamezingira eneo lote la chuo na
wanafunzi wapo mabwenini.
No comments:
Post a Comment