UZINDUZI WA SHERIA NDOGO WA MFUKO WA AFYA YA JAMII WILAYANI USHETU MKOANI SHINYANGA

Mgeni
Rasmi ,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Benson Mpesya akisisitiza
jambo kwa wadau kuhusiana na umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya
Jamii (CHF) katika uzinduzi wa sheria ndogo ya Mfuko huo wilaya Usheto.

Mwakilishi
wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bwana
Constantine Makala akiwasalimia wadau wa Wilaya ya Ushetu baada ya
kukaribishwa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Ushetu.

Afisa
Masoko na Elimu kwa Umma kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hawa
Duguza, akiwasilisha mada ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa wadau
katika uzinduzi wa sheria ndogo ya Mfuko wa Afya Ya Jamii wilyani
Usheto.

Meneja
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Shinyanga, Bwana Imanuel Amani
akisisitiza umuhimu wa wana ushetu kujiunga na mfuko wa Afya ya
Jamii(CHF) katika shughuli ya wadau wa Mfuko huo wilayani Usheto.

Wadau wakifuatilia kwa makini mada iliyokua ikiwasilishwa na Afisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
…………………………………………………………………….
…………………………………………………………………….
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika kutekeleza majukumu yake ya
kuhakikisha wananchi wengi wananufaika na bima ya Afya umeshirikiana na
Halmashauri ya wilaya ya Ushetu mkoani Shinyanga kuanzisha sheria ndogo
ya Mfuko wa Afya ya Jamii(CHF)
Uzinduzi
wa mchakato wa kuanzisha sheria ndogo uliambatana na siku ya wadau wa
afya wilayani ushetu ambao umefanyika katika ukumbi wa halmshauri ya
wilaya na mgeni rasmi alikuwa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Benson
Mpesya.
Katika
uzinduzi huo kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mh.Benson Mpesya alisitiza
kuhusu umuhimu wa viongozi wa mkoa na wadau wa afya kuhakikisha
wananchi wanajiunga kwa wingi kwenye mfuko huu kwani ndio mkombozi wa
Afya zao.
No comments:
Post a Comment