PICHA:WAZIRI MKUU MSTAAFU NA MBUNGE WA MONDULI EDWARD LOWASSA ASHIRIKI MAZISHI YA JOHN NYERERE BUTIAMA

Mtoto
wa mwisho wa marehemu John Guido Nyerere anayefahamika kwa jina la
Wanzagi akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na shangazi yake Anna
Nyerere.

Lowassa akisaliama na mmoja wa viongozi wa dini mkoani Mara.


Edward Lowassa (MB) akisaliama na baadhi ya wananchi wa Mwitongo, Butiama baada ya kushiriki mazishi ya John Nyerere jana

Mbunge wa Monduli akimfariji kaka wa Marehemu, madaraka Nyerere.

Lowassa akisalaimana na wananchi wa Mwitongo.

Mbunge
wa Monduli na waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akimfariji Mjane wa
baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere kufuatia kifo cha mtoto wake John
Nyerere wakati wa mazishi ya mtoto huyo wa nne wa Nyerere katika kijiji
cha Mwitongo, Butiama, mkoani Mara jana

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akizungumza na Mbunge wa
Jimbo la Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowassa wakati wa
mazishi ya John Guido Nyerere yaliyofanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa
,Butiama.

Ni huzuni kwa kila mtu.

Askari wa JKT wakiwa na mashada ya maua mbele ya jeneza lililo na mwili wa Mpiganaji Vita ya Kagera, Marehemu John Nyerere.

Askofu
wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mhashamu Michael Msonganzila
akitoa heshima za mwisho kwa marehemu John Guido Nyerere baada ya
kukamilika kwa ibada maalum iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki
la Bikira Maria wa Damu Azizi ya Yesu Jimbo la Musoma Parokia ya
Butiama.

Jeneza
lenye mwili wa marehemu John Guido Nyerere likiteremshwa kaburini na
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Mama Maria Nyerere akiweka udongo kwenye kaburi la mtoto wake John Guido Nyerere.

Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Asha-Rose Migiro akiweka udongo kwenye kaburi la John Guido Nyerere.

Mama Maria Nyerere akiweka shada la mau kwenye kaburi la mtoto wake John Guido Nyerere.

Mtoto
wa Marehemu anayeishi Lusaka Zambia, Sofia Nyerere Mwape akiweka shada
la maua kwenye kaburi la Baba yake marehemu John Nyerere.
No comments:
Post a Comment