JAMBO LEO YAICHABANGA BODABODA FC TAMASHA LA BODABODA UKONGA
Mlinda
mlango Maganga Benjamin wa timu ya Bodaboda Wilaya ya Ilala, akiudaka
mpira katikati ya wachezaji wa timu ya Jambo Leo 'Wagumu Stars' Zahoro
Mlanzi (kushoto) na Ali Salum wakati wa Tamasha la Bodaboda
lililofanyika kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam. Mgeni
rasmi katika tamasha hilo alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry
Silaa. Jambo Leo ilishinda mabao 2-1.
Mchezaji wa timu ya Jambo Leo, Frank Balile (kushoto) akiwania mpira na mchezaji wa timu ya Bodaboda, Sharif Mohamed
Moja ya kizazaa langoni mwa Bodaboda FC iliyosababishwa na washambuliaji wa Jambo Leo
Mshambuliaji
wa timu ya Gazeti la Jambo Leo, Ali Salum (katikati) akifunga bao la
kwanza dhidi ya Bodaboda FC,wakati wa Tamasha la Bodaboda lililofanyika
kwenye Uwanja wa Ukonga Gerezani, Dar es Salaam leo. Mgeni rasmi katika
tamasha hilo alikuwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa.Jambo Leo
ilishinda mabao 2-1.
No comments:
Post a Comment