ZIARA YA WAZIRI WA ARDHI MH. WILLIAM LUKUVI BABATI MKOANI MANYARA

Mkuu
wa mkoa wa Manyara ,Mhe.Joel Nkaya Bendera akizungumza katika kikao cha
viongozi wa wilaya zote za mkoa huo kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa
Mkoa mjini Babati,kushoto ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya
Makazi,Mhe.William Lukuvi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati,Crispin
Meela.Mhe.Bendera amesisitiza nidhamu ya kazi katika kuhudumia wananchi
na ameapa kuwaondoa watendaji wabovu mkoani humo.

katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa wa Manyara kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati.Ameuagiza uongozi wa mkoa huo kumaliza migogoro ya ardhi ifikapo mwezi Mei mwaka huu.

Mratibu
wa Tume ya Waziri Mkuu ya kuhakiki na kuweka mipaka kwenye maeneo yenye
migogoro ya ardhi mkoani Manyara,ambaye pia ni Mrasimu Ramani
Mwandamizi,Bw.Benedict Mugambi akitoa maelezo ya hatua waliyofikia
katika kuweka mipaka mkoani Manyara na kusema kuwa migogoro mingi ya
mipaka inasababishwa na wanasiasa. 

Baadhi
ya watendaji wa sekta ya Ardhi Kanda ya Kaskazini na baadhi ya
waheshimiwa wabunge akiwemo Mbunge wa Kiteto,Benedct Ole Nangoro na
Mbunge wa Viti Maalum,Pauline Gekul wakifatilia maelekezo ya Mhe Lukuvi
alipozungumza na watendaji wa mkoa wa Manyara jana.
No comments:
Post a Comment