ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE NDANI YA JIMBO LA LONGIDO MKOANI ARUSHA.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi na bendera za
aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Longido ambaye amejiunga
na CCM kwenye mkutano uliofanyika Eworendeke.Ndugu Kinana akiwa
ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wako kwenye
ziara ya siku tisa mkoani Arusha ya Kuhimiza,kuimarisha na kutekeleza
Ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka 2010 ikiwemo pia na kusikiliza
matatizo ya Wananchi na kuyapatia ufumbuzi.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia wilayani humo.

Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Eworendeke
ambapo alitoa salaam za shukrani kwa CCM wilaya ya Longido kwa kuipa
ushindi mzuri wakati wa uchaguzi.

Wananchi wakisikiliza hotuba kwa makini.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ujenzi
wa nyumba ya watumishi wa Afya katika kijiji cha Lesingeita,wilayani Longido.Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Longido Mh.Lekule Laizer.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Eworendeke
ambapo alimpongeza mbunge wa jimbo la Longido kwa uamuzi wake wa
kutogombea uchaguzi ujao na kusema wanasiasa wengi wanajua kuingia
kwenye siasa lakini wakisahingia hawajui wakati gani wa kutoka.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi
wa Kijiji cha Engikareti wilaya Longido.

Mzee
Kitasho Simel Nakutamba akimpa mkono Katibu Mkuu wa CCM ndugu
Abdulrahman Kinana mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika hoteli
yake ya Longido kama ionekanavyo pichani.

Pichani ni jengo la kituo cha mafunzo cha Learning In Longido (LIL),ambapo Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana aliweka jiwe la msingi na kushiriki kupaka rangi kwenye
majengo hayo.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi kwenye
majengo ya kituo cha mafunzo cha Learning In Longido (LIL).

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiandaa sindano ya
chanjo tayari
kwa kumchoma ng'ombe.,Pichani shoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Arusha,Ndugu Onesmo Ole Nangolo akishuhudia tukio hilo.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kumchoma ng'ombe chanjo
kwenye mradi wa ufugaji wa madume bora katika kijiji cha Ketumbeine.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya
ufunguzi wa jengo la hoteli katika kijiji cha Kitumbeine,kushoto ni
mmiliki wa hoteli hiyo Ndugu Halifa Juma.

Mbunge wa Viti Maalumu Vijana,Catherine Magige akiwahutubia wakazi wa Eworendeke,Wilayani Longido.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vijana wa kimasai
alipowasili kwenye kituo cha mafunzo Learning In Longido
No comments:
Post a Comment