jamii inapaswa kuwekeza katika sayansi na teknolojia - Balozi Sefue
Mgeni
rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na wajumbe wa
warsha wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ya ubunifu wa sera ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia iliyoandaliwa na Wizara ya Mawasilano,Sayansi na
Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi katika ufunguzi wa warsha ya ubunifu wa sera ya Taifa katika
Sayansi na Teknolojia Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue(katika)
akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia
Prof. Patrick Makungu(kushoto), na Naibu Katibu Mkuu wa Hiyo John
Mngodo,warsha hito iliandaliwa iliandaliwa na Wizara ya
Mawasilano,Sayansi na Teknolojia jijini Dar es Salaam.
Na May-Zuhura Simba
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kuwa ili jamii iweze kukua
kwa kasi na kupata maendeleo haina budi kuwekeza katika sayansi na
teknolojia.
Aliongea
hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya kupitia
marejeo ya mfumo wa Taifa wa sayansi,teknolojia na ubunifu ulioandaliwa
na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
“ubunifu
katika sayansi na teknolojia ni kitu muhimu katika kupata uvumbuzi wa
vitu mbalimbali muhimu vinavyoleta maendelao kwa jamii husika hivyo kuna
umuhimu wa kuwafungia wanasayansi katika atamizi ili kupata matokeo
mazuri ya utafiti” alisema Balozi Sefue.
Aidha
aliongeza kuwa nchi kama Korea na Singapore waliwekeza katika
sayansi,technologia na ubunifu na hivyo kujikwamua kiuchumi na kuleta
maendeleo kwa jamii zao.
Vilevile
alisisitiza kuwa ubunifu ukisimamiwa dhabiti utasaidia katika kuleta
mageuzi kwenye sekta muhimu ikiwemo elimu, afya,biashara,kilimo na
miundombinu na hivyo kutatua matatizo ya kijamii.
“Mfano
mzuri ni Max malipo ambalo ni zao la vijana wa kitanzania waliokuwa
wamewekwa katika atamizi na kuleta uvumbuzi huu kwa kutumia sayansi na
teknolojia ” alisema Balozi Sefue.
Aidha
aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo,makampuni binafsi, na serikali
kushirikiana kwa pamoja kufungua vituo atamizi zitakavyosaidia vijana
kuvumbua teknolojia mbalimbali.
No comments:
Post a Comment