Header Ads

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA WAWEKEZAJI NA MARAIS WA NCHI 5 ZA AFRIKA MASHARIKI.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akitoa taarifa ya mkutano wa wawekezaji (Round Table Investment Forum) na wakuu wa nchi 5 za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia  Machi 25 hadi 26 mwaka huu.
Kamishina wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova akitoa taarifa ya hali ya ulinzi na usalama katika jiji la Dar es salaam na vifo vya watu  7 waliopoteza maisha  kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa  zinazoendelea kunyesha katika jiji la Dar es salaam. 
Na Aron Msigwa –MAELEZO.

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa wawekezaji (Round Table Investment Forum) na Marais wa nchi 5 za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia  Machi 25 hadi 26 mwaka huu.  

Akitoa taarifa ya mkutano huo Mkuu wa wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki  amesema kuwa Marais hao Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo watahudhuria mkutano huo wakiwa wameambatana na  jumla ya wawekezaji 350. 
Amesema Tanzania kwa mara nyingine imepata heshima ya kuandaa mkutano huo na kufafanua  kuwa wawekezaji hao wamekwisha anza  kuwasili jijini Dar es salaam kuanzia  Machi 22 , Machi huku marais nchi hizo wakitarajiwa kuwasili jijini humo kuanzia Machi 24,2015.

No comments:

Powered by Blogger.