RAIS KIKWETE AMPONGEZA RAIS MPYA WA NAMIBIA DKT.HAGUE GEINGOB

Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Rais Mpya wa Namibia Dkt.Hage
Geingob wakati wa sherehe za kuapishwa kwake zilizofanyika katika
Uwanja wa michezo wa Uhuru wa Namibia jijini Windhoek leo.Sherehe za
kumuapisha Rais huyo wa tatu wa Namibia ziligongana na maadhimisho ya
miaka 25 ya uhuru wan chi hiyo.
(picha na Freddy Maro)
………………………………………………………………………………….
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumamosi, Machi 21, 2015, ameungana na viongozi mbalimbali wa
Afrika na wananchi wa Namibia katika kusherehekea miaka 25 ya uhuru wa
nchi hiyo na kuapishwa kwa Rais wa Tatu wa Namibia, Mheshimiwa Dkt. Hage
Gotfried Geingob.
Mheshimiwa
Geingob alikuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo kabla ya uchaguzi mkuu wa
Novemba 28, mwaka jana, uliokipa ushindi mkubwa chama tawala cha SWAPO.
Katika
sherehe kubwa na ya kufana iliyofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa
Independence mjini Windhoek, Rais Kikwete ameshuhudia Namibia
ikiadhimisha miaka 25 ya Uhuru wake na makabidhiano ya uongozi wa juu wa
nchi hiyo kwa amani kwa mara ya pili katika historia yake.
Mheshimiwa
Dkt. Geingob ameapishwa rasmi na Jaji Mkuu wa nchi hiyo, Mheshimiwa
Peter Shivute saa sita na dakika 25 kwa saa za Afrika Mashariki, kiapo
ambacho kilifuatiwa na kiapo cha Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Naibu
Waziri Mkuu.
Ujumbe
wa Tanzania katika sherehe hizo uliwashirikisha pia marais wa zamani,
Mzee Ali Hassan Mwinyi na Rais Ben Mkapa, ambao wote waliwasili mjini
Windhoek usiku wa jana kwa ndege maalum ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment