Muswada wa Sheria ya Udhibiti wa Umiliki Silaha wasomwa kwa mara ya Pili Bungeni
bu Waziri wa Mambo
ya Ndani Mhe.Pereira Silima amesoma Muswada wa Sheria ya Kupendekeza kutungwa kwa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha ya
mwaka 2014 Bungeni Dodoma kwa mara ya pili tarehe 19 Machi 2015.
Mhe.Silima alisema Serikali imeona umuhimu wa kutunga Sheria
hii ya Udhibiti wa Umiliki wa silaha
kutokana na kukabiliana na tatizo la kuwepo na watu wengi wanao kumiliki silaha
kinyume na sheria pamoja na kufanya matumizi mabaya ya silaha.
“Serikali imekubaliana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki kuwa na mfumo wa kisheria baada ya kusaini na kuridhia maazimio ya kudhibiti
uzagaaji wa silaha haramu na sheria hii
inaelekeza wazi kuwa mtu anaweza kumiliki silaha akiwa na umri wa kuanzia miaka
25,”alisema Mhe.Silima.
Mhe.Silima aliendelea
kusema kuanzia mwaka 2000 mpaka 2013 serikali ilikamata zaidi ya silaha 34,156
zilizokamatwa katika operesheni mbalimbali na silaha hizo ziliteketezwa.
Kwa upande wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama inayoongozwa
na Mhe.John Chiligati aliipongeza serikali kupitia kifungu chake cha 19
kinachoeleza kuwa sihala zote zitawekwa alama ya utambuzi wa kitaifa,Pia baada
ya sheria hii kupitishwa suala hilo lizingatiwe.
“Kamati inapenda kuishauri Serikali katika kifungu cha 20(2) kuondoa
adhabu ya kulipa faini kwa mtu anayemiliki silaha kinyume na sheria na badala yake
ni kutumikia kifungu kisichozidi miaka mitano”,alisema Mhe.Chiligati.
Mhe.Chiligati aliendelea kusema kamati imeridhia marekebisho
ya Serikali ya kuongeza idadi ya wajumbe wa kamati ili iwe na uwakilishi mpana kutoka sekta binafsi,Pia Kamati imeshauri
kifungu cha 5(3) kisomeke kuwa mtu
yeyote atakuwa na sifa za kuteuliwa kuwa mjumbe wa kamati endapo ni raia wa
Jamhuri ya Muungano.
Naye Mbunge wa Nkasi Kusini Mhe.Desderius Mipata ameipongeza
Serikali kwa kuunda Sheria itakayo dhibiti umiliki wa silaha nchini, pia ameishauri serikali kuangalia ni
namna gani itadhibiti maduka yanayouza silaha nchini.
No comments:
Post a Comment