Rais Kikwete akagua vijiji vilivyoathiriwa na Mvua Chalinze

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
mkewe Mama Salma wakiwasili kwa helikopta katika kata ya Chalinze
wakitokea jijini Dar es Salaam jana, kukagua uharibifu ulioletwa na mvua
kubwa iliyoambatana na upepo mkali na kuharibu makazi ya watu na
kujeruhi ambapo kaya 47 zikiathirika katika vijiji vya Msoga na Tonga.(picha zote na Freddy Maro)

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na
mkewe Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wa kata Ya Chalinze
wakikagua baadhi ya nyumba zilzoharibiwa vibaya baada ya kuangukiwa na
miti kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha katika
kata ya Chalinze na kuathiri kaya 47.Rais Kikwete alikagua uharibifu
huo, kuzungumza na kuwafariji wana vijiji hao na kuahidi kuwasaidia
katika janga hilo

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakizungumza na wana vijiji waliopatwa na dhoruba la mvua.


Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwafariji wana vijiji hao na kuahidi kuwasaidia katika janga hilo
Na Freddy Maro Chalinze,Bagamoyo.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
jana aliwafariji na kuahidi kuzisaidia kaya 40 ambazo nyumba zao
ziliharibiwa vibaya na mvua mkubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki
iliyopita huko Chalinze,wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Katika ziara hiyo Rais Kikwete ambaye alikuwa amefuatana na mkewe mama Salma Kikwete alikagua Shule ya msingi Chalinze, Ofisi ya CCM, na nyumba kadhaa za wanakijiji ambazo ziliharibiwa vibaya na mvua hizo na kujeruhi baadhi ya wanavijiji walioangukiwa na nyumba zao.
“Nimepata taarifa ya maafa yaliyotokea, sikuwepo kwahiyo
nimekuja kuwapa pole.Poleni sana Kwa wale ambao nyumba zimeharibika
serikali inao utaratibu wa kusaidia.Mkurugenzi akipata taarifa atajua
jinsi gani ya kuwasaidia.Lakini kuna misaada tunayoweza kutoa.Nasikia
Mbunge ametoa msaada wa chakula na dawa pamoja na matibabu.
Lakini Kwenye
serikali tunao wajibu wetu.Mkurugenzi yupo taarifa zipilekwe kwake kwa
uhakika ilitujue la kufanya.Poleni sana tutaendelea kusaidiana,” alisema
Rais Kikwete ambaye pia ni Mkazi wa kijiji cha Msoga, kata ya Chalinze.
Mvua mkubwa iliyoambatana na upepo mkali wiki liyopita iliharibu kabisa majengo nane katika kata ya Chalinze ambapo kuta zilibomoka mabati kuezuliwa na upepo mkali na miti kuangukia nyumba na kujeruhi wana kijiji kadhaa ambao walitibiwa katika hospitali ya Tumbi.Kaya 47 kutoka vijiji vya Msoga na Tonga ziliathirika na mkasa huo.
No comments:
Post a Comment