ZANZIBAR YAZINDUA CHANJO YA SURUA NA RUBELLA.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt. Jamala Adam Taib akielezea
utaratibu wa kampeni ya chanjo ya Surua na Rubela pamoja na matone ya Vitamin A
na dawa za minyoo itakavyoendeshwa katika uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo kitaifa uliofanyika kijiji cha Uroa Mkoa wa Kusini
Unguja.
Wazazi na wanafunzi wa kijiji cha
Uroa waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Surua na Rubela
wakimsikiliza mgenai rasmi katika uzinduzi huo Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud
Thabit Kombo (hayupo pichani) kabla ya uzinduzi wa Chanjo hizo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo ya Surua na Rubella Naibu
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akimpatia mtoto matone ya Vitamine A katika
uzinduzi wa chanjo hiyo kitaifa uliofanyika
kijiji cha Uroa.
Muuguzi wa Kituo cha Afya cha Uroa akimpatia mtoto chanjo ya surua na
Rubella kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika kijijini hapo. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
No comments:
Post a Comment