CHOMBO CHOCHOTE KITAKACHO KIUKA MAADILI YA HABARI KUKIONA CHAMOTO
Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Juma
Nkamia akitoa hutuba
yake kwenye uzinduzi wa Nembo ya radio Triple A fm na kuwataka wamiliki
na wanahabari kuhakikisha wanafuata maadili ya taaluma ya uandishi wa
habari iwe kazini au nje ya
kazi zao.
Serikali
imesisitiza kuwa haitavifumbia macho vyombo vya habari vitakavyo kiuka
maadili ya habari na kuwa haitasita kuvichukulia hatua kali vyombo
hivyo.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari vijana utamaduni na michezo
Juma Nkamia wakati akizindua logo ya redio Triple A fm jijini hapa huku
akiwataka wanahabari kuzingatia maadili ya kazi zao iliwaweze kuitumikia
jamii
bila ya kuleta uchochezi kwa jamii utakaopelekea uvunjifu wa
amani.
Naibu Waziri wa habari vijana utamaduni na
michezo Juma Nkamia akiwa na
Bodi ta wakurugenzi wa Kampuni ya The Blue Triple A Ltd ambayo ni
kampuni tanzu ya Radio Triple A fM inayoongozwa na Mkurugenzi wake kulia
na kushoto Mr&Mrs Papa King Mollel wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya naibu waziri kuzindua nembo ya Radio hiyo jijini
hapa
Nkamia alisema kuwa Taaluma hiyo inaweza kuileta jamii katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili uaoendelea hapa nchi au kuzidi kuumomonyoa maadili hayo kwani wao kazi yao ni kuhabarisha kuelimisha na kuburudisha jamii inayovizunguka vyombo hivyo hivyo vinamchango mkubwa katika maendeleo ya taifa.
"Lengo
hapa ni kuhakikisha kuwa vymbo vya habari haviwi ndio kichocheo cha
uvunjifu wa amani ila nawasihi muwe kichocheo katika suala zima la
kupiga vita mmomonyoko wa maadili yetu kwa nyinyi mpo karibu zaidi na
jamii"alisisitiza Nkamia
No comments:
Post a Comment