MWIMBAJI NYOTA WA MUZIKI WA INJILI ROSE MUHANDO KUZINDUA KAMATA PINDO MIKOA 10
MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili Tanzania, Rose Muhando anatarajia kuzindua albamu yake ya Kamati Pindo yenye nyimbo nane atakayoifanya kwenye mikoa zaidi ya 10 ya Tanzania bara, uzinduzi utakaofanyika Agosti mwaka huu. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama awali uzinduzi wa albamu hiyo ulikuwa ufanyike kabla ya Tamasha la Pasaka lilimalizika Mei 4 jijini Mwanza, kutokana na unyeti wake wameonelea kufanikisha baada ya tamasha.
Msama alisema uzinduzi wa albam hiyo utakuwa ni wa Kimataifa kwa sababu utashirikisha waimbaji mbalimbali kutoka nje ya Tanzania, hivi sasa taratibu za uzinduzi huo zinafanyika. “Katika uzinduzi huo, Rose Muhando ataimba live nyimbo zake zote tangu alipoanza kazi ya uinjilishaji, hasa kwa nyimbo zake kama Mteule uwe macho, Nibebe na nyinginezo ambazo atapiga live siku hiyo,” alisema Msama.
Albam hiyo ya Kamata Pindo la Yesu imefanikishwa na kampuni ya Msama Promotions ikiwa ina nyimbo ambazo ni Facebook, Wewe Waweza, Nibariki, Kwema, Muongo, Usiniache, Bwana Niongoze na iliyobeba albam ambayo ni Kamata Pindo la Yesu.
Rose Muhando anatamba na albam zake nyingine zilizofanya vizuri ambazo ni pamoja na Mteule uwe Macho, Nibebe, Utamu wa Yesu, Jipange Sawasawa, Mungu anacheka na y a sasa ambayo ni Kamata Pindo la Yesu.
No comments:
Post a Comment