KINANA AWAKUTANISHA HAMIS KIGWANGALAH NA HUSSEIN BASHE WILAYANI NZEGA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akisalimiana na wananchi
wa katika mkutano wa hadhara wa CCM katika Kata ya Ndala, wilayani
Nzega, Tabora leo, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua
miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM na kukagua
maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na kusikiliza kero za
Wananchi.
Mbunge wa Jimbo la Nzega Hamis Kigwangalah (kushoto), akimpongeza Mjumbe
wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Hussein Bashe aliyetoa mchango wa sh.
50,000 za kusaidia ujenzi wa jengo la CCM tawi la Puge, wilayani Nzega
leo.
Wakazi wa Kata ya Ndala, wilayani Nzega. wakishangilia kwa kuonesha
ishara ya CCM wakati wa mkutano wa hadhara katika kata hiyo,
uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) akijadiliana
jambo na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa, Hussein Bashe walipokutana
wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM wilayani Nzega.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana 9kulia) akisaidiwa na Mbunge wa
Jimbo la Nzega, Hamis Kigwangalah kujenga jengo la Hospitali ya Wilaya
ya Nzega.
Kinana akisalimiana na wasanii wa ngoma ya asili waliotumbuiza wakati wa ujenzi wa jengo la ofisi ya CCM Kata ya Nkiniziwa
Kinana akizungumza baada ya kukagua maabara katika Shule ya Sekondari
ya Kampala, katika Kata ya Ndala, wilayani Nzega, Tabora. Kutoka kushoto
ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, Hussein Bashe na Mbunge wa
Jimbo la Nzega.
No comments:
Post a Comment