KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AKAGUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO NA KUFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA WILAYANI NZEGA LEO
Katibu mkuu wa ccm,Ndugu Abdulrahman Kinana akipita kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la
mapokezi la wagonjwa wa nje (OPD),hospitali ya wilaya ya Nzega,mapema leo mchana,katika ziara yake anayoendelea nayo yenye
lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali
sambamba na wananchi,ikiwemo pia kusikiliza kero za wananchi zinazowakabili na
kuzitafutia majibu.
Katibu mkuu wa ccm,Ndugu Abdulrahman Kinana kulia na Mbunge wa
jimbo la Nzega,Mh.Hamisi Kingwangalla wakishiriki katika ujenzi wa jengo la
mapokezi la wagonjwa wa nje (OPD),hospitali ya wilaya ya Nzega,wakati Ndugu
Kinana alipokagua ujenzi wa jengo hilo katika ziara yake anayoendelea nayo yenye
lengo la kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali
sambamba na wananchi,ikiwemo pia kusikiliza kero za wananchi zinazowakabili na
kuzitafutia majibu.
Katibu
mkuu wa ccm,Ndugu Abdulrahman Kinana akioneshwa jambo kwenye simu na
mfuasi wa chama cha CCM,mapema leo,wakati Ndugu kinana alipokwenda
kushiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM kata katika kijiji cha
Nkiniziwa,Wilayanni Nzenga mkoani Tabora.
Katibu mkuu wa ccm,Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM kata katika kijiji cha
Nkiniziwa,Wilayani Nzenga mkoani Tabora. 

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani shoto na Katibu wa NEC
Siasa,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakimsikiliza mwanafunzi wa kidato cha nne
shule ya sekondari ya Kampala,Amos Kashindye namna ya kutumia moja ya kifaa cha
maabara,mara baada ya kuitembelea shule hiyo ya kata na kukagua maabara ya sayansi
na fizikia katika shule hiyo.
Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Ndala katika mkutano wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa Taifa,wilayani Nzega mkoani Tabora.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akikagua moja ya barabara
zinazojengwa mjni Nzega kwa kiwango cha lami,kushoto kwake ni Katibu wa NEC
Itikadi,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye na pichani kati ni Mkuu wa Mkoa wa
Tabora,Mh,Fatma Mwasa.
Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na
Uenezi,Nape Nnauye akiyapokea baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na baadhi
ya vijana wanaojishughulisha na uchimbaji wa madini wilayani Nzega,wakiomba
Serikali na chama cha CCM,kuwasaidia vijana hao wachimbaji wadogo wadogo kupewa
maeneo yao ya kuchimba madini bila kubugudhiwa na mengineyo

Sehemu
ya Wananchama na wafuasi wa chama cha CCM,wakiwa kwenye mkutano wa
hadhara wa chama hicho uliofanyika Nzega mjini mapema leo.
Nape
Nnauye akiwahubia Sehemu ya Wananchana na wafuasi wa chama cha
CCM,katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Nzega mjini
mapema leo.
Baadhi
ya Baiskeli zilizotolewa na Mjumbe wa Mkutano Halmashauri kuu CCM
Taifa,Ndugu Hussein Bashe kwa ajili ya kuwakabidhi viongozi wa
mbalimbali wa chama hicho katika suala zima la kurahisha utendaji wao wa
kazi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahubia baadhi ya Wananchana na wafuasi wa
chama cha CCM,katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Nzega
mjini mapema leo.
Sehemu
ya Wananchama na wafuasi wa chama cha CCM,wakimsikiliza Katibu MKuu wa
CCM,Ndugu Kinana (hayupo pichani) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara
wa chama hicho uliofanyika Nzega mjini mapema leo.
Mkuu wa mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akizungumza jambo kwenye mkutano wa hadhara wa CCM,uliofanyika jioni ya leo Nzega Mjini.

Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimpongeza Mjumbe wa Mkutano mkuu wa
CCM,Taifa,Ndugu Hussein Bashe mara baada ya kukabidhi piki piki tatu kwa
jumuiya za Chama,na Baiskeli 163 kwa ajili ya matawi yote ya CCM ya
Wilaya ya Nzega kupitia mradi wao wa kuimarisha chama,pia alitoa
baiskeli 37 kwa Jumuiya ya UVCCM wilayani humo,Pia alikabidhi kiasi cha
shilingi Milioni mbili kwa kikundi cha Boda boda na milioni mbili kwa
kikundi cha Mamalishe.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimpongeza Mbunge wa Nzega,Mh.Hamisi
Kingwangalla mara baada ya kukabidhi mashine ya kutotolea vifaranga kwa
kikundi cha vijana.
No comments:
Post a Comment