DAR YAZIZIMA KUFUATIA KIFO CHA BALOZI FLOSSIE GOMILE CHIDYAONGA
Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Zanzibar (Muungano na Utawala Bora), Mh. Mwinyi
Haji Makame, akisaini kitabu cha maombolezo mara baada ya kuwasili
kuhudhuria misa maalum ya kumwombea aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini,
Mh Flossie Gomile Chidyaonga kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa
Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Zanzibar (Muungano na Utawala Bora), Mh.
Mwinyi Haji Makame akibadilishana mawazo na Balozi wa Nigeria nchini
Tanzania Dk Ishaya Samaila Majanbu (kushoto).
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb), akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu
Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. John Haule na
kulakiwa na Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb), akisubiri kwenda kutia saini kitabu cha maombolezo kabla ya kuanza
kwa ibada maalum ukumbini hapo. Kushoto ni Makamu Balozi wa Malawi
nchini Tanzania, Mh. Chisiza.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb), akisaini kwa huzuni Kitabu cha Maombolezo kufuatia kifo cha
aliyekuwa Balozi wa Malawi hapa nchini, Hayati Flossie Gomile-Chidyaonga
kilichotokea Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam tarehe 09 mei
2014. Kulia ni Makamu Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Mh. Chisiza.


Balozi wa Finland Tanzania, Sikka Antila wakilia kwa uchugu pamoja na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, Bi .Joyce Mends-Cole wakati wa misa maalum ya kumwombea aliyekuwa balozi wa Malawi nchini Tanzania Mh. Flossie Gomile Chidyaonga kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment