Balozi wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Flossy Gomile-Chidyaonga afariki dunia jijini Dar es salaam leo
“Ni kwa masikitiko makubwa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa (ya Malawi) unauarifu umma kufariki dunia kwa Balozi Flossy
Gomile-Chidyaonga baada ya kuugua kwa muda mfupi jijini Dar es salaam mchana
huu”, imesema taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara hiyo Quent Kalichero.
“Tangu mwaka 2006 Marehemu Bi Flossy Gomile-Chidyaonga alikuwa
Naibu Balozi wa Malawi London kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini
Tanzania mnamo Septemba mwaka 2011”, imesema taarifa hiyo na kuongezea kuwa
taratibu za mazishi zitatangazwa baada ya taratibu kukamilika.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MALI PEME PEPONI-AMEN
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MALI PEME PEPONI-AMEN
No comments:
Post a Comment