Taarifa ya Habari Kutoka ITV LEO: Imetokea milipuko miwili kwa wakati mmoja katika maeneo tofauti mjini zanzbar na kusababisha hofu kubwa kwa wananchi wa mji mkongwe ambapo mlipuko mmoja ulitokea hoteli ya mercury iliyopo forodhani na wa pili umetokea kanisa la anglikana eneo la mkunazini.
Eneo ambalo limeharibika kwa kuchimbika na kitu cha mripoko katika eneo la mkunazini, na kuleta mtafaruku na tukio hilo la mripuko katika majira ya mchana, Katika mripuko huo hakuna mtu aliyepata majarana na uharibifu wa majengo katika eneo hilo.
Maofisa wa JWTZ wakiangalia eneo la tukio lililochimbika kutokana na kitu kinachodhaniwa ni bomu, katika tukio hilo hakuna Mwananchi aliyejeruhiwa
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Kiongozi wa Kanisa la Mkunazini Ndg. Nuhu Salanya, na Maofsa wa JWTZ , katika eneo la tukio na kutowa maelekezo kwa Uongozi wa Kanisa alipofika katika eneo la tukio kuangalia athari na uharibifu uliotokea katika eneo hilo, wakati wa mripuko huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Makamanda wa JWTZ waliofika eneo la tukio kuagalia na kuchunguza tukio hilo la mripoko katika eneo la Mkunazini jirani la Kanisani.
No comments:
Post a Comment