Picha Kutoka IKULU:VIONGOZI WAPYA WA IKULU SACCOS WAJITAMBULISHA KWA KATIBU MKUU KIONGOZI NA OMBENI SEFUE NA KUKABIDHI RIPOTI YA UTENDAJI.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Watatu
kushoto) akiwa pamoja na Viongozi wa Ikulu SACCOS wakati walipokwenda
kujitambulisha na kukabidhi ripoti ya utendaji ofisini kwake ikulu jijini Dar
es Salaam jana.Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa SACCOS hiyo Bwana
Theofrid Kikombele, Wapili kushoto ni Katibu wa SACCOS hiyo Bwana David
Kivembele na kulia ni mshauri mkuu wa SACCOS hiyo Bwana Joseph Sanga.

Viongozi wa Ikulu Saccos wakiwa kwenye
mkutano na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ofisini kwake ikulu jijini
Dar es Salaam janai.Picha na Freddy Maro-IKULU
--
Uongozi
Mpya wa ikulu SACCOS jana umejitambulisha rasmi kwa Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue, ikulu jijini Dar es Salaam na kukabidhi ripoti ya
utendaji ya SACCOS hiyo.
Waliojitambulkisha
kwa Katibu Mkuu Kiongozi ni pamoja na Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS Bwana
Theofrid Kikombele,Makamu Mwenyekiti Bwana David Kivembele na Mshauri
Mkuu Bwana Joseph Sanga.
Akizungumza
mara baada ya kujitambulkisha, Mwenyekiti wa SACCOS hiyo Bwana Theofrid
Kikombele alisema uongozi huo umepanga mikakati madhubuti ya kuiendesha
SACCOS hiyo kwa uwazi na ufanisi zaidi ikizingatia kutenda kazi kwa
weledi na kuwahamasisha wafanayakazi wengi zaidi kujiunga.
Mkakati
mwingine, alisema Bwana Kikombele ni kwa SACCOS hiyo kuanzisha vitega
uchumi mbalimbali kwa lengo la kupanua mtaji ili kuweza kuwahudumia
vyema wanachama wa SACCOS hiyo kwa kuwawezesha kukopa zaidi kwaajili ya
shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo.
Wakati
wa mkutano huo kati ya Katibu Mkuu na Uongozi wa Saccos hiyo Viongozi
hao walikabidhi ripoti ya utendaji wa SACCOS hiyo na walimuomba Katibu
Mkuu Kiongozi kujiunga na SACCOS hiyo, ombi ambalo aliliafiki na kuahidi
kutoa ushirikiano kuboresha SACOSS hiyo.
No comments:
Post a Comment