Picha:Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa Azindua Rasmi Kampeni Za Ubunge Jimbo la Kalenga

Picha Juu ni bango litakalo tumiwa kumuuza mgombea wa CHADEMA Bi Tendega Grace Mvanda
kwenye uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi
Machi 16, 2014 CHADEMA inataraji kuzindua kampeni zake jimboni Kalenga tarehe
22 Februari 2014.


msafara wa CHADEMA ukiongozwa na katibu mkuu wa chadema Dk Wibrod Slaa Ukielekea kuzuru kaburi la Chief Mkwawa
kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara ambapo viongozi na wanachama
ambao walikuwa hawajawahi kufika hapo walipata baraka za wana ukoo wa
chifu huyo aliyeandika historia mujarabu ya eneo hilo.
Mvua ni
kubwa sana lakini watu wanavumilia mvua hiyo bila kujali huku
wakionyesha mapenzi yao kwa chama chao na mbunge wao mtarijiwa anaye
kwenda kuziondoa kero za wanakalenga zilizodumu kwa zaidi ya miaka 50 ya
uhuru.Picha na Habari-Chadema
---
Kama
mnavyojua kuwa jana CHADEMA kilizindua kampeni zake kwenye Jimbo la
Kalenga, uzinduzi utao ongozwa na katibu mkuu wa chama na nguli wa siasa
za Tanzania Bwana Dr Wilbroad Slaa utakata utepe kusafisha njia ya
kwenda kuchaguliwa Bi Grace Mvanda anayeeperusha bendera ya CHADEMA
kwenye uchaguzi unao tarajiwa kufanyika tarehe 16 Machi 2014.
No comments:
Post a Comment