Header Ads

KAMPUNI YA MONABAN YAKABIDHI MSAADA WILAYA YA HAI KWA AJILI YA WAHANGA WA MAAFA



DSCF2880Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichopo jijini Arusha Bw.Philemon Mollel akimkabidhi Mkuu wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga msaada wa Tani nne za unga  wenye thamani ya shilingi Milioni 4.2,baada ya wilaya yake kupata maafa yaliyotokana na mvu zilizoambatana na upepo mkali na kusababisha badhii ya watu kukosa nyumba za kuishi
DSCF2878Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga Arusha Philemon Mollel akiongea mbele ya wanakijiji(hawapo pichani)namna alivyoguswa na maafa hayo yaliyopelekea kutoa msaada huo huku kiwataka wafanyabishara,makampuni,watu binafsi kujitokeza kuwasaidia waanga wa maafa hao,mbali na msaada huo wa tani nne za unga pia alitoa shilingi Milioni moja kwaajili ya waanga.

DSCF2866Kina mama ambao ndio waathirika wa kubwa wa maafa hayo wakisubiria zoezi la kugawiwa chakula cha msaada 
DSCF2870Mtendaji wa kijiji Bi.Trea Ramadhani akitoa shukrani zake za dhati kwa mmiliki wa kiwanda cha kuzalisha unga kilichipo Arusha.

DSCF2882Mkuu wa wilaya Novatus Makunga akimkabidhi msaada uliotolewa na kampuni ya Monaban ,mtendaji wa kijiji cha  kwa sadala Bi.Trea Ramadhani msaada uliogharimu zaidi ya milioni 4,Kushoto ni kaimu mkurugenzi Bw.Zabdieli Moshi
DSCF2883Mkuu wa wilaya ya Hai Mh.Novatus Makunga akitoa shukrani zake za dhati kwa mmiliki wa kiwanda cha Monaban kwa kuweza kuwaletea chakula cha msaada na kuwataka makampuni,mashirika na watu binafsi kuiga mfano wa Monaban kwa kuwasaidia waanga wa maafa yaliyotokana na mvua zilizoambatana na upepo mkali na kusababisha watu kukosa makazi hivi karibuni ktika wilaya yake.

No comments:

Powered by Blogger.