SERIKALI KUONDOA TATIZO LA MAJI MKOA WA IRINGA
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Uwezeshaji Dk. Mary Nagu akiwasili katika viwanja
vya bunge mjini Dodoma mapema hii leo tayari kwa kuhudhuria mkutano wa
kumi na tatu kikao cha nne.
Mbunge
wa Kilolo Mh. Peter Msolla (kulia)akiingia katika ukumbi wa Bunge hii
leo tayari kuhudhuria mkutano wa kumi na tatu kikao cha nne, katikati
ni Mbunge wa Sikonge Mh. Said Nkumba na kushoto ni Mbunge wa Kigamboni
Mh. Dk. Faustine Ndugulile.
Picha zote na Eliphace Marwa, MAELEZO Dodoma
Frank Mvungi-Maelezo Dodoma
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kutatua tatizo la maji
katika mji wa mafinga Mkoani Iringa ili kuwapa fursa wananchi kujiletea
maendeleo kwa haraka.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kasim Majaliwa wakati akijibu swali la
mbunge wa Mufindi Kaskazini mh.Mahmoud Hassan Mgimwa aliyetaka kujua
hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuondoa tatizo la maji katika
jimbo la Mufindi.
Alieleza
kuwa mradi wa upanuzi wa mradi wa maji katika mji wa Mafinga
unakadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 60 ambapo mradi huo
utasaidia kuondoa tatizo hilo katika mji wa Mafinga.
Katika
mradi huo Mh. Majaliwa alibainisha kuwa Serikali kupitia Wizara ya Maji
imefanya usanifu wa mradi mkubwa ambao utahusisha ujenzi wa bwawa lenye
ukubwa wa ujazo wa lita zipatazo milioni 2,800,000 ili kukidhi mahitaji
yaliyopo.
Aidha
Mh. Majaliwa aliongeza kuwa mradi huo utahusisha ujenzi wa tanki 1 la
mita za ujazo 1000 eneo la changarawe,Luganga tanki 1 la mita za ujazo
225 na mtula ujenzi wa tanki 1 la mita za ujazo 1000.
Pia
Mamlaka ya Maji Mafinga kwa kushirikiana na Wizara ya Maji pamoja na
Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) ipo katika mpango wa kukopa
kiasi cha zaidi ya milioni 300,000 kutoka katika taasisi za fedha kwa
ajili ya kuboresha huduma ya maji katika mji wa mafinga kwa kufanya
upanuzi na uboreshaji wa miundombinu ya maji iliyopo.
Mji
wa Mafinga una jumla ya wakazi 51,902 ambapo kabla ya kutekelezwa kwa
mradi huu wananchi wanapoata huduma ya maji na salama ni asilimia 63

No comments:
Post a Comment