Header Ads

DKT.MVUNGI APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU ZAIDI

DKT. Sengondo Mvungi akiwa amepakiwa kwenye ndege leo kuelekea nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

=======  =======  =======

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dk. Sengondo Mvungi aliyekuwa akipata matibabu katika Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) baada ya kuumizwa vibaya na majambazi, amesafirishwa leo, Novemba 7, 2013) saa 5:45 asubuhi kwenda nchini Afrika Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi.

Taarifa iliyotolewa na Tume hiyo, imesema, akiwa nchini Afrika Kusini, Dkt. Mvungi atapata matibabu katika Hospital ya Milpark iliyopo jijini Johannesburg.

"Itakumbukwa kuwa Dk. Mvungi alivamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia sJumapili, Novemba 3, 2013. Tukio hilo la uvamizi linaendelea kuchunguzwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini", ilisema taarifa hiyo.

Imesema tangu siku alipojeruhiwa, Dk. Mvungi alikuwa akipata matibabu katika Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI). Hata hivyo, Madaktari waliokuwa wakimtibu MOI, walishauri afanyiwe uchunguzi na matibabu zaidi. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Dk. Mvungi ameondoka na ndege ya kukodi ya Shirika la Ndege la Flightlink na ameambatana na Dk. Mugisha Clement Mazoko kutoka MOI, Muuguzi Bi. Juliana Moshi, na mtoto wa kaka yake Bw. Deogratias Mwarabu NA KWAMBA Serikali inagharamia gharama zote za matibabu ya Dk. Mvungi.

Tume imewaomba wananchi wote waendelee kumuombea kwa Mungu Dk. Mvungi ili aweze kurejea katika hali yake ya kawaida na hatimaye kuendelea majukumu yake.

No comments:

Powered by Blogger.