Zawadi za Rock City Marathon 2013 zawekwa hadharani
Mratibu
wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (kulia) akipokea
mfano wa tiketi ya ndege kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika
la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana (kushoto), ambayo
itatolewa kwa mshindi wa mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02
iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za kilometa 21 za Rock City
Marathon mwaka jana. PW pia ni msafirishaji mkuu wa mbio za Rock City
Marathon 2013. Wapili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa
Precision Air, Bi. Linda Chiza, na Meneja Matukio wa kampuni ya Capital
Plus International Ltd, Bi. Grace Sanga
Mkurugenzi
wa Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick
Ndekana (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
juu ya udhamini wa shirika lake katika mbio hizo kama wasafirishaji
wakuu katika mbio hizo na kutoa tiketi bure kwa mshindi wa mwaka huu
atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita katika mbio za
kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana. Kulia ni Mratibu wa mbio
hizo Bw. Mathew Kasonta aliyetangaza zawadi zilizoboreshwa kwa mshindi
wa mwaka huu, na kushoto ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa
Precision Air, Bi. Linda Chiza
Mratibu
wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (Kulia)
akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kutangaza
zawadi za mbio za Rock City Marathon mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana ambaye
alieleza juu ya udhamini wa shirika lake katika mbio hizo kama
wasafirishaji wakuu katika mbio hizo na kutoa tiketi bure kwa mshindi wa
mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita
katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana
Mratibu
wa mbio za Rock City Marathon 2013, Bw. Mathew Kasonta (wapili kulia)
akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kutangaza
zawadi za mbio hizo kwa mwaka huu. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa
Biashara wa Shirika la Ndege la Precision Air (PW), Bw. Patrick Ndekana ambaye
alieleza juu ya udhamini wa shirika lake katika mbio hizo kama
wasafirishaji wakuu katika mbio hizo na kutoa tiketi bure kwa mshindi wa
mwaka huu atakaevunja rekodi ya 1:04:02 iliyowekwa na Kopiro Mwita
katika mbio za kilometa 21 za Rock City Marathon mwaka jana. Kushoto ni
Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa Precision Air, Bi. Linda Chiza na
kulia ni Meneja Matukio wa kampuni ya Capital Plus International Ltd,
Bi. Grace Sanga.
====== ======= ========
Zawadi za Rock City Marathon 2013 zatangazwa
Waandaji
wa mbio za Rock City Marathon 2013, kampuni ya Capital Plus
International (CPI) wametangaza kutenga shilingi milioni kumi kama
zawadi katika mbio hizo zilizopangwa kufanyika mwezi Oktoba tarehe 27
katika viwanja vya CCM Kirumba mkoani Mwanza.
Katika
kunogesha mbio hizo na kuifanya iwe ya ushindani zaidi, shirika la
ndege la Precision Air (PW), mbali na kuwa wasafirishaji wakuu wa Rock
City Marathon 2013, limetangaza kutoa tiketi ya kwenda na kurudi jijini
Dar es Salaam kwa mshiriki atakaevunja rekodi ya muda wa 1:04:02
iliyowekwa na Kopiro Mwita katika kilometa 21 mwaka uliopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wa kutangaza
zawadi hizo, Mratibu wa mbio hizo Bw. Mathew Kasonta alisema zawadi kwa
mbio za mwaka huu zimeboreshwa zaidi na kuongeza kuwa washindi katika
mbio za kilometa 21 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia shilingi
milioni 1.5/- kila mmoja, 900,000/- kwa washindi wa pili na 700,000/-
kwa washindi wa tatu.
“Tunahamasisha
washiriki kujitokeza kwa wingi kwa sababu zawadi kwa mbio za mwaka huu
zimeboreshwa baada ya kupata mwitikio mzuri kutoka kwa wadhamini wetu
ambao ni NSSF, Africa Barrick Gold (ABG), Precision Air, Airtel, Bank M,
PPF, Nyanza Bottling Ltd, New Mwanza Hotel, Sahara Communications,
Continental Decoders na Umoja Switch,” alisema Bw. Kasonta.
Kasonta
alisema washindi katika kilometa 5 wa mbio maalum kwa wafanyakazi
kutoka makampuni mbali mbali, watapatiwa zawadi za kiheshima na fedha
wakati washindi kwenye mbio za kilometa 3 ambazo washiriki wake ni wazee
na watu wenye ulemavu wa ngozi wataondoka na zawadi ya shilingi elfu
50,000/- kwa mshindi wa kwanza, 30,000/- kwa wa pili na 20,000/- wa
tatu.
“Kwa
mbio za kilometa 2 kwa watoto kati ya umri wa miaka 7 mpaka 10, mshindi
atajinyakulia shilingi elfu 30,000/-, 20,000/- kwa mshindi wa pili na
15,000/- kwa mshindi wa tatu,” aliongeza.



No comments:
Post a Comment