WATANZANIA WAHUDHURIA MKUTANO WA JUMUIYA YA MADOLA
Kutoka
kushoto ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dkt. Philip
Mpango, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile, Kamishna
wa Sera Bw. Beda Shallanda na Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Said Magonya
wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa majadiliano ya mkutano wa
madola.
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa majadiliano ya Jumuiya ya Madola.
Mwenyekiti wa majadiliano ya mkutano wa Madola Bw. Sheku Sesay akifafanua jambo. Picha zote na Bi. Eva Valerian – Washington DC.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia majadiliano; mwenye tai nyekundu ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile./
====== ======= ========
WATANZANIA WAHUDHURIA MKUTANO WA JUMUIYA YA
MADOLA
Wakati
mikutano mingine ikiendelea hapa mjini Washington DC, Tanzania pia inashiriki
katika mkutano wa Jumuiya ya Madola ambao utafanyika kwa siku mbili mfululizo.
Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe wote ambao ni nchi wanachama.
Katika
mkutano huo kikubwa kilichojadiliwa ni kuhusiana na suala zima la biashara, ni
namna gani biashara inaweza kufanyika na kwamba nchi zetu haziko vizuri sana
katika uwanja huu wa kimataifa. Katika mkutano huo walijadili ni jinsi gani
wanaweza kufanikisha lengo la kuanzisha mfuko ambao utatumika kusaidia biashara
‘trade facilitation’.
Katika
majadiliano yaliyokuwa yakifanyika wajumbe wengi walipenda kujua kwamba ni
tofauti gani mfuko huo mpya utaleta ili nchi zetu ziweze
kunufaika. Hiki ni kitu kikubwa zaidi kilicho wagusa wajumbe wengi.
Akizungumza
na vyombo vya habari Dkt. Silvacius Likwelile ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
ambaye alisema kuwa”katika mkutano huu jambo ambalo limezungumziwa sana ni kuhusu kuondoa
vikwazo ambavyo mara nyingi tunawekewa ili kufikia masoko katika ulimwengu”. Aliendelea
kusema kuwa, ni imani yetu kwamba tume ya madola itafanyia kazi masuala hayo
ili hatimaye tuwe na msimamo mmoja wa kuweza kusaidia ukuaji wa biashara katika
nchi zetu. Mkutano
huu utaendelea tena kesho na inategemewa utakuwa na mafanikio makubwa.
Imetolewa na:
Ingiahedi
Mduma
Msemaji
Mkuu
Wizara
ya Fedha
Washington
D.C
08/10/2013
No comments:
Post a Comment