UZINDUZI WA KAMPENI YA "TUSOME TANZANIA" NA RAIS MSTAAFU BENJAMINI W. MKAPA MAKTABA YA MKOA LEO JIJINI DAR.
Rais Mstaafu Mhe. Benjamini William
Mkapa ambaye pia ni mgeni rasmi akihutubia vijana mbalimbali wakati wa uzinduzi
wa Kampeni ya tusome Tanzania (Let us read Tanzania) aliyoizindua leo katika viwanja
vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vijana walioshiriki
uzinduzi wa Kampeni ya tusome Tanzania (Let us read Tanzania) wakifuatilia kwa
makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Mhe. Benjamini William Mkapa (hayupo pichani)
leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wadau toka timu ya Let us
read Tanzania akimpa maelezo juu ya vitabu mbalimbali viliyotungwa na waandishi
mashuhuri ndani na nje ya nchi.
Rais Mstaafu Mhe. Benjamini William
Mkapa ambaye pia ni mgeni rasmi akiwasomea hadithi mbalimbali na kuwauliza
maswali mbalimbali watoto ambao ni wanafunzi toka shule mmbalimbali leo katika
viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.
PICHA ZOTE NA BENEDICT
LIWENGA-MAELEZO.
====== ======== =======
RAIS MSTAAFU
MHE. BENJAMINI WILLIAM MKAPA AZINDUA KAMPENI YA TUSOME TANZANIA (LET US READ
TANZANIA CAMPAIGN).
Na Benedict
Liwenga-Maelezo, Dar es Salaam.
11/10/2013.
RAIS Mstaafu Mhe. Benjamini William
Mkapa amezindua rasmi Kampeni ya “Tusome Tanzania (Let’s read Tanzania Campaign)
iliyoandaliwa na wadau mbalimbali nchini wenye lengo la kuwahamasisha vijana wa
kitanzania kujijengea utamaduni wa kusoma vitabu mbalimbali.
Katika uzinduzi huo, Mhe. Mkapa
ameipongeza kamati ya wadau waandaaji wa kampeni hiyo kwa kujitoa kwao katika
kuhakikisha kuwa watoto wa shule ambao ndiyo taifa la kesho wanapata kujionea
wenyewe na anatumaini kuwa watahamasika kupenda kujisomea kwa manufaa ya maisha
yao.
“Tabia ya kusoma inamjenga mtu
kifikra na kumpa mtu mtazamo”. Alisema Mhe. Mkapa. Mhe. Mkapa ameongeza kuwa kwa kuwa
elimu haina mwisho, kusoma ni namna ya kujielimisha siku hadi siku na kufungua
mambo mapya yanayoipa akili changamoto, hivyo amewasisitizia vijana wajijengee
utamaduni wa kusoma hasa vitabu vya kiswahili na Kiingereza.
“Someni kazi za Shaabani Robert
mwandishi mkongwe wa Tanzania, someni
kazi za Mariam Abdallah, Ngugi wa Thio’ngo , Chinua Achebe, Ole Soyinka na .”
Alisema Mhe. Mkapa.
Aidha, Mhe. Mkapa ametoarai kwa wadau
waandalizi wa kampeni ya “Let’s read Tanzania Campaign” kuwa zoezi hilo lisiishie hapo bali liwe
endelevu na kuwafikia watu wengi na haswa vijana, pia amesisitiza kuwa mtandao
wa vitabu uhakikishe vitabu hivi vinafika hadi kwenye shule za vijijini na
amehamisisha juu ya ujenzi wa Maktaba na kusaidia kuboresha watoto wetu.
Let’s read Tanzania Campaign ni
kampeni iliyoandaliwa na vijana kutoka hasasi mbalimbali lenye lengo la
kuwahamasisha vijana wa kitanzania kujijengea utamaduni wa kupenda kusoma
vitabu kwa ajili ya kuongeza fikra za vijana na kuwasaidia katika maisha yao.




No comments:
Post a Comment