Naibu Mwakilishi wa Shirika la Hans Sedel Kanda ya Afrika Mashariki Konrad akimkabidhi moja ya stika za kupamba na rushwa Kamishna
wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja wakati wa
hafla fupi ya Makabidhiano ya nakala 10600 za vitabu vya Haki na ulinzi
wa mtoto, Fahamu misingi ya amani na usalama katika familia pamoja na
stika 4000 za kupambana na rushwa zilizochapishwa na shirika hilo.Kulia
ni Mkuu wa huduma za Polisi Jamii Naibu Kamishna Michael Kamhanda.
Naibu
Mwakilishi wa Shirika la Hans Sedel Kanda ya Afrika Mashariki Konrad
akimkabidhi moja ya kitabu cha Haki na ulinzi wa mtoto Kamishna wa
Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja wakati wa hafla
fupi ya Makabidhiano ya nakala 10600 za vitabu vya Haki na ulinzi wa
mtoto, Fahamu misingi ya amani na usalama katika familia pamoja na stika
4000 za kupambana na rushwa zilizochapishwa na shirika hilo kwa lengo
la kulisaidia jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu jijini Dar es
Salaam jana.Kulia ni Mkuu wa huduma za Polisi Jamii Naibu Kamishna
Michael Kamhanda.
Naibu
Mwakilishi wa Shirika la Hans Sedel Kanda ya Afrika Mashariki Konrad
Teichert akizungumza katika hafla fupi ya Makabidhiano ya nakala 10600
za vitabu vya Haki na ulinzi wa mtoto, Fahamu misingi ya amani na
usalama katika familia pamoja na stika 4000 za kupambana na rushwa.Kulia
ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja
pamoja na Mkuu wa huduma za Polisi Jamii Naibu Kamishna Michael
Kamhanda.
---
Na Tamimu Adam, Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi limekabidhiwa zaidi ya nakala 10600 za vitabu vya Polisi jamii na ulinzi shirikishi kutoka shirika la Hans Sidel Foundation ambavyo
vitatumika katika kuendelea kuhamasisha dhana ya Polisi jamii na ulinzi
shirikishi pamoja na kuendeleza mpango wa kufikisha elimu ya usalama
hadi ngazi ya familia.
Nakala za vitabu zilizokabidhiwa ni kitabu cha Haki na Ulinzi wa mtoto, nakla 5300 na kitabu cha fahamu misingi ya amani na usalama katika familia nakala 5300 pamoja na stika 4000 za kupambana na rushwa.
Vitabu hivyo vilikabidhiwa na Mwakilishi wa shirika la Hans Sidel Bw. Konrad Teichert na
kupokelewa na Kamishina wa Opereheni na Mafunzo (CP) Paul Chagonja kwa
niaba ya Jeshi la Polisi katika hafla fupi iliyofanyika jana Makao makuu
ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es salaam.
Chagonja
alisema kuwa vitabu hivyo vimefika wakati muafaka ambapo Jeshi la
Polisi linaendelea na mpango wake wa kufikisha elimu ya usalama hadi
ngazi ya familia pamoja na mapambano dhidi ya rushwa ambayo kila mmoja
anatakiwa kuwajibika ili kutokomeza rushwa hapa nchini.
Aliongeza kuwa vitabu hivyo vinalenga katika kuimarisha ulinzi shirikishi na kuwawezesha kila
mmoja katika familia kuwezeshwa na kujengewa uwezo katika kubaini na
kuzuia fursa za kutendeka kwa uhalifu au vurugu ndani ya jamii.
Kwa
upande wake Mwakilishi wa shirika la Hans Sidel Bw. Konrad Teichert
alisema wataendelea kushirikiana na jeshi la Polisi katika kusaidia
kufanikisha maboresho ya jeshi hilo pamoja na kuendelea kufanya mafunzo
ya kuwajengea uwezo Maofisa na Askari wa Jeshi la Polisi.
Naye
Mkuu wa Ufuatiliaji na tathimini wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishina wa
Polisi, (DCP) Omar Rashid alishukuru shirika la Hans Sidel kwa
ushirikiano walioutoa katika kusaidia kuchapisha vitabu hivyo na
kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo , maofisa, wakaguzi na askari,
ambapo jumla ya wahitimu 17 walitunukiwa vyeti vya mafuzo hayo.
No comments:
Post a Comment