SEKTA BINAFSI YAASWA KUJA NA HUDUMA ZINAZOKIDHI WATU WA KIPATO CHA CHINI
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Uchukuzi na
Usalama kutoka Wizara ya Uchukuzi, Bi. Tumpe Mwaijande akizungumza na
wageni waalikwa wakati wa ufunguzi rasmi wa bidhaa mpya kabisa ya bima
nchini Tanzania “Safari Njema” mahsusi kwa wasafiri.
.Ndege Insurance na African Life Assurance waja na “Safari Njema Bima” mahsusi kwa wasafiri
.kila msafiri anaweza kukata bima ya maisha safari njema inayotoa kinga ya siku 7 awapo safarini
.Mwaka jana pekee ajali 23,000 watu waliopoteza maisha 5,320
Na Damas Makangale, Moblog
SERIKALI imeitaka sekta binafsi katika
usafiri na usafirishaji kuja na bidhaa huduma ambazo zinamlenga mtu wa
kipato cha chini na zinakidhi mahitaji ya wananchi katika juhudi za
kuboresha maisha ya watanzania kupitia sekta ya uchukuzi nchini. Moblog
linaripoti.
Akizungumza na wageni waalikwa wakati wa
ufunguzi rasmi wa Bima ya Safari Njema jijini Dar es Salaam leo,
Mkurugenzi wa Uchukuzi na Usalama toka Wizara ya Uchukuzi, Bi Tumpe
Mwaijande ambaye alikuwa anasoma hotuba ya Waziri Dk Harrison Mwakyembe
amesema sekta ya uchukuzi ni nguzo muhimu katika kusukuma mbele gurudumu
la maendeleo kwa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
“tunawashukuru African life Assurance na
Ndege Insurance Brokers kwa kuja na huduma hii mpya kwa wananchi lenye
lengo la kupunguza machungu na makali ya maisha endapo itatokea ajali au
ulemavu wakati wa safari, huu ni mfano wa pekee katika ushirikiano kati
ya serikali na sekta binafsi katika kumletea mwananchi maendeleo,”
amesema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ndege Insurance
Brokers, Dk Sebastian Ndege akitoa hotuba yake na kuelezea jinsi huduma
hii ya safari njema bima itakavyofanya kazi kwa wasafiri hapa nchini.
Amesema Serikali kupitia Wizara ya
Uchukuzi inaendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kuhakikisha
maisha ya watanzania yanalindwa wakati wapo safarini kwa kuwaletea bima
ya safari njema yenye bei na viwango nafuu ili kumwezesha mtu wa kipato
cha chini kumudu gharama hizo.
Mwaijande amesema taifa kila siku
kupoteza nguvu kazi kwa sababu ya ajali za mara kwa mara ambazo wahanga
wa ajali mara nyingi kuachwa bila fidia lakini baada ya uzinduzi huu wa
bima ya safari njema kwa wasafiri ni mkombozi wa kweli kwa watanzania.
“Huduma hii ya Safari njema bima kwa
wasafiri nchini ni mkombozi wa kweli kwa wahanga wa ajali endapo
itatokea ulemavu au kifo kwa wasafiri basi wanaweza kufidiwa au
kutibiwa,”alisisitiza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa
Ndege Insurance Brokers, Dk Sebastian Ndege amesema vifo na ulemavu
vitokanavyo na ajali ni moja kati ya adui mkubwa wa maendeleo ya
mtanzania.
Afisa Mtendaji Mkuu wa African Life
Assurance, Ndg Julius Magabe akizungumza na wageni waalikwa wakati
uzinduzi rasmi wa bidhaa mpya ya safari njema bima kwa watanzania jijini
Dar es Salaam katika stendi ya mabasi Ubungo.
Amesema kuwa endapo itatokea kifo, mrithi
alietajwa atalipwa Tsh 10m na ulemavu wa kudumu mbima atalipwa kiasi
cha Tsh 10m kwa kupitia njia rahisi ya (Mobile Money) kama vile Mpesa,
Tigopesa, Airtel Money na Zpesa.
“Takwimu zinazonyesha, kati ya Januari na
Disemba 2012, zilitokea ajali 23,000 ambapo watu wapatao 5,320
walipoteza maisha na ukichukua wastani wa utegemezi wa watu wanne kila
marehemu mmoja, ni sawa na wahanga elfu ishirini kwa kila mwaka
‘Pale unapokua safarini, unachotakiwa
kufanya ni kupiga kwenda number Nyota -150-nyota-23-alama ya reli na
utapata maelezo ya BIMA hii ni jinsi ya kujiunga utahitajika kujaza
taarifa muhimu kama jina lako, tarehe ua kuzaliwa, jina la mrithi na
namba yake ya simu,” amesema Ndege
Dk Ndege amesema Ndege insurance kwa
kushirikiana na African Life Assurance imeona umuhimu wa kubuni bidhaa
inayomjali mtanzania wa kipato cha chini kuweza kumudu Bima za ajali
safarini kwa bie nafuu.
Dk Ndege aliendelea kusema kuwa kupitia
bidhaa yao mpya wamejiandaaa kutoa elimu kwa umma ju ya umuhimu wa BIMA
ya maisha kwa watanzania na pia kuhakikisha inapatikana kwa urahisi na
wananchi.
Mwenyekiti wa Bodi ya African Life
Assurance na Waziri wa Zamani Ibrahim Kaduma akizungumza na wageni
waalikwa na kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa shughuli
hiyo.
Akiielezea bima ya safari njema, Bw
Julius Magabe, Afisa Mtendaji Mkuu wa African Life Assurance, amesema
uanzishwaji wa bima ya safari njema unaendana na dhima ya African life
ya kuboresha maisha ya watanzania kupitia upatikanaji wa bima za maisha.
“Ni matazamio yangu kuwa, kiwango kidogo
cha ukataji wa bima ya safari njema cha shilling 5,000 kitawawezesha
watanzania wengi kuipata huduma hii muhimu kwa wasafiri wa mbali na hata
wale waendao kwenye shughuli za kila siku,” amesema Magabe
Ndege Insurance Brokers kwa kushirikiana
na African life Assurance kampuni ya bima ya maisha wamezindua rasmi
huduma ya bima ya maisha kwa wasafiri wa mabasi, magari, daladala, meli
na ndege. Bima hii ya maisha yenye kutoa mafao kwa watakaokata bima
wakati wakisafiri.
Safari Njema ndio jina maalumu bima hii
ya maisha ya wasafiri, sasa kila msafiri anaweza kukata bima ya maisha
safari njema inayotoa kinga ya siku 7 uwapo safarini.
Picha juu na chini ni baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa Safari Njema huduma mpya ya bima kwa wasafiri nchini.
Mgeni rasmi Bi Tumpe Mwaijande akikata
utepe kuashiria huduma mpya ya Bima ya wasafiri "Safari njema"
imezinduliwa rasmi jijini Dar leo, Kulia ni Dk. Sebastian Ndege na
Julius Magabe.
Mgeni rasmi Bi Tumpe Mwaijande akifungua kitambaa cha utepe wakati wa uzinduzi.
Sasa imezinduliwa rasmi Watanzania kazi kwenu jali maisha yako na familia yako pindi unaposafiri itakugharimu Tshs 5000/=.
Dr. Sebastian Ndege akipeana mkono na Mgeni rasmi Bi.Mwaijande.
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya
Ryan Bert and Compay Limited na Swordfish Security Consultants Haki
Ngowi (mwenye miwani mweusi) naye alikuwa ni miongoni mwa wageni
waalikwa kwenye uzinduzi huo.
Mgeni rasmi Bi. Mwaijande akiondoka eneo la tukio baada ya uzinduzi.
Afisa Mtendaji Mkuu wa African Life
Assurance Ndg Julius Magabe na Mkurugenzi Mtendaji wa Ndege Insurance
Brokers, Dk Sebastian Ndege wakipeana ya kheri baada uzinduzi wa Huduma
yao mpya ya Bima ya Safari njema katika soko la Tanzania.
Dk Sebastian Ndege akibonyeza mashine
ya kodi maalumu EFD toka TRA wakati wa uzinduzi rasmi wa safari njema
bima ambayo ni bidhaa mpya katika soko la Tanzania.
Wakili Justin Ndege (kulia) akiwa na wadau wengine wakati wa uzinduzi wa bima ya Safari njema.
No comments:
Post a Comment