Header Ads

NMB YATOA MSAADA HOSPITALI YA WILAYA ILEJE 
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Janet Mbene akishukuru uongozi wa benki ya NMB kwa msaada wa mashuka na vitanda vya akina mama katika  hospitali ya Itumba  wilaya ya Ileje .Msaada huo wenye thamani ya shilingi milioni Tano umetolewa na benki ya NMB kupitia tawi la Ileje mwishoni mwa wiki katika viwanja vya hospitali ya Itumba.

                                                                             
                                                                                          
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ileje, Nd. Mohamed Mwala akimshukuru Meneja wa Kitengo cha Huduma za Serikali  wa NMB , Bw. Elieza Msuya  baada ya kupokea msaada wa vitanda na mashuka ya hospitali ya wilaya ya vilivyotolewa na benki ya NMB.  Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Janet Mbene


 Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Janet  Mbene akimshukuru Meneja wa Kitengo cha Huduma za Serikali  wa NMB , Bw. Elieza Msuya  baada ya kupokea msaada wa vitanda na mashuka ya hospitali ya  Itumba  wilaya ya Ileje vilivyotolewa na benki ya NMB.   

No comments:

Powered by Blogger.