Header Ads

MAHAFALI YA KWANZA YA SHULE YA WAMA NAKAYAMA YATIKISA NYAMISATI RUFIJI

1Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mama Salma Kikwete Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo WAMA wakati alipowasili katika viwanja vya mahafali katika mahafali ya Kwanza ya Shule ya Sekondari WAMA Nakayama yaliyofanyika katika shule hiyo iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani jana.Zaidi ya wanafunzi 60 walitunukiwa vyeti vya kumaliza kidato cha nne na zawadi mbalimbali zilitolewa kwa wahitimu wakati wa mahafali hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na viongozi na watu mashuhuri akiwemo balozi wa Japan na wafanyabiashara ambapo mwenyekiti wa IPP Reginald Mengi aliahidi kuisadia shule hiyo shilingi milioni 200 kila mwaka kwa miaka mitano mbazo ni kiasi cha shilingi bilioni moja kwa miaka hiyo mitano.1aaRais Jakaya Kikwete akizungumza na wageni waaikwa na wahitimu wakati wa mahafali hayo jana huko Nyamisati Rufiji. 2Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa shule ya WAMA Nakayama Suma Mensa na viongozi mbalimbali wakati aliowasili shuleni hapo. 4Watu mashuhuri na viongozi mbalimbali wakiwa katika mahafali hayo 5Mama Salma Kikwete akiwasili katika eneo la tukio kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya shule hiyo Dr. Ramadhan Dau. 5aWahitimu wakiingia katika eneo la tukio 6Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma kikwete akicheza na wanawake wenzake wake wa viongozi. 6bRais Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akiwa na viongozi mbalimbali katika meza kuu wakiimba wimbo wa taifa uliooongozwa na wanafunzi wa shule ya WAMA Nakayama kutoka kulia ni Balozi anzania Mhe.Masaki Okada Mkuu wa mkoa wa Pwani Ndugu Mwantumu Mahiza, Mama Salma Kikwetena kutoka kushoto ni Dr. Ramadhan Dau Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Wama Nakayama na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa. 7Baadhi wa walimu wa shule hiyo 7cBaadhi ya wanakamati kutoka kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, Daudi Nasibu katibu mkuu taaisis ya WAMA na Dan Kiondo. 8Baadhi ya wananfunzi wa shule ya WAMA Nakayama 8cMh. Mbunge Vick Kamata akiongoza wanafunzi wa Wama Nakayama kuimba wimbo maalum kwa wahitimu katika mahafali hayo

No comments:

Powered by Blogger.