KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AZINDUA MPANGO MKAKATI WA PILI WA BOHARI YA DAWA (MSD)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Charles Pallangyo akizindua mpango
mkakati wa pili wa bohari ya dawa MSD unao tarajiwa kuanza julai 2014
hadi juni 2020 wenye lengo la kuongeza ubora kiutendaji katika uzinduzi
uliofanyika kwenye hoteli ya Hyyat Regency jijini Dar es salaam jana.Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Charles Pallangyo
akizungumza na Katibu Mkuu Wizara ya TAMISEMI Bw Deo Mtasiwa mara baada
ya kuzindua mpango huo jana katikati ni Kamimu Mkurugenzi wa Bohari kuu
ya dawa (MSD) Bw. Cosmas MwaifwaniKamimu Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa (MSD) Bw. Cosmas Mwaifwani akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es salaamBaadhi ya wadau waliohudhuria katika uzinduzi huoBaadhi ya wafanyakazi wa MSD wakiwa katika hafla hiyoMgeni
Rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Bw. Charles
Pallangyo akiwa katika picha ya pamoja na wageni waalikwa mbalimbali
mara baada ya uzinduzi huo
…………………………………………………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
MAFANIKIO
ya kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa nchini ni matokeo ya kuisha kwa
mkakati wa kwanza ulianza julai mosi 2007 na kumalizika Juni 30 mwaka
huu imefahamika.
Hayo
yalibainishwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Charles
Pallangyo Dar es Salaam jana, wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau
kujadilimpango mkakati wa pili bohari ya dawa MSD unao tarajiwa kuanza
julai 2014 hadi juni 2020 wenye lengo la kuongeza ubora kiutendaji
,kutoa huduma na kukuza mtaji wa bohari ya dawa.
”
Mpango mkakati wa kwanza ulileta mafanikio makubwa kwa kupunguza
upungufu wa dawa nchini na kupanuka kwa maghala katika makao makuu na
ofisi za kanda” alisema Pallangyo.
Aliongezea
kuwa mpango mpya 2014-2015 unatarajia kutekeleza malengo mbalimbali
yakiwemo kuongeza imani kwa wateja, kupunguza gharama na kuboresha
mazingira ya kazi.
Katika
hatua nyingine MSD, wameweka malengo katika mpango mkakati ambayo ni
kuongeza upatikanaji wa dawa kwa silimia 95 , kuongeza upatikana kwa
huduma kwa wateja kwa asilimia 100, kuongezeka kwa soko kwa asilimia 80,
kuanzisha secta binafsi katika uzalishaji wa dawa ndani na nje ya nchi
na kuboresha mahusiano na wadau kwa asilimia 95.
Mwenyekiti
wa bodi ya wadhamini wa MSD, Idris Mtulia alisema kuwa bohari ya dawa
inampango wa maendeleo unaolenga kuboresha na kuleta ufanisi katika
utendaji kazi ambayo hupangwa kila baada kipindi fulani.
Mtulia
aliongezea kuwa, mpango mkakati wa pili umetayarishwa kwa kutumia mfumo
wa usimamizi wa utendaji kazi unaojulikana kama mfumo mizania, una
lengo la kusimamia, kufuatilia na kutathimini utekelezaji wa mpango
Mkakati ili kuhakikisha huduma hiyo inafika kila pembe ya nchi yetu.
No comments:
Post a Comment