DKT. SHEIN ASISITIZA AMANI BARAZA LA IDD ZANZIBAR
Baadhi ya Wananchi waliohudhuria katika swala ya Idi –El –Hajji iliosaliwa Kitaifa huko katika kitongoji cha Marumbi Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja.
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akiwapamoja na viongozi na
wananchi mbalimbali katika Swala ya Idi –El-Hjji ilioswaliwa Kitaifa
huko katika kitongoji cha Marumbi Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja.
Baadhi
ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria katika Baraza la Idi-El-Hajji
lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja
Rais
wa Zanzibar Dk Ali Mohd Shein wapili kushoto akiomba Dua pamoja na
viongozi wengine wa Kitaifa katika Swala ya Idi –El-Hjji ilioswaliwa
Kitaifa huko katika kitongoji cha Marumbi Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati
Unguja.kulia kwake ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Khamis Haji Khamis na
kushoto yake ni Katibu mtendaji wa Wakfu na Mali ya Amana Sheikh Abdalla
Twalib,Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanizbar Maalim Seif Sharif Hamadi
na wamwisho ni Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Mahmod Mussa Wadi.
Rais
wa Zanzibar D kali Mohd Shein kulia akiwa pamoja na Makamo wa Kwanza wa
Rais Maalim Seif Sharif Hamad mara baada ya kumalizika kwa Baraza la la
Idi -El-Hajji lililofanyika huko Tunguu Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati
Unguja
========= ======== ========
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 16/01/2013.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali
Mohamed Shein ameendelea kusisitiza hali ya Amani na kukemea Vitendo
vinavyofanywa na baadhi ya Watu wachache wenye lengo la kuiharibu sifa ya
Zanzibar.
Amesema tangu Karne zilizopita Zanzibar pamekuwa pahala pa Amani
na utulivu na hivyo kuitaka jamii kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa vyombo
vya ulinzi na usalama ili kuwafichua watu ambao wanaoharibu Amani iliyopo.
Rais Shein ameyasema hayo leo katika Hotuba yake aliyoitoa
katika Baraza la Idd lililofanyika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Tunguu Mkoa wa
Kusini Unguja.
Amesema kiujumla hali ya Amani na Utulivu imetanda kote katika
Visiwa vya Zanzibar hali inayopelekea Serikali kupanga na kutekeleza mipango
yake ya kimaendeleo kwa lengo la kuimarisha uchumi na ustawi wa Wananchi wake.
Hata hivyo amekea tabia inayofanywa na baadhi ya Watu wachache
wanaowahujumu na kuwatia hofu Wananchi pamoja na Wageni wanaoitembelea
Zanzibar.'
Amefahamisha kuwa hakuna Dini inayowaelekeza waumini wake
kuwahujumu Wanadamu wengine na kwamba watakaobainika kufanya vitendo hivyo
watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Amewahahakikishia Wananchi na Wageni kwamba vyombo vya Ulinzi na
usalama vinafanya kazi nzuri ya kusimamia ulinzi na Usalama na kuitaka jamii
kutoa ushirikiano unaohitajika.'
Aidha Dkt. Shein amebainisha kuwa kutokana na kuimarika kwa hali
ya usalama na amani Uchumi wa Zanzibar unaendelea kukua kwa kiwango cha
kuridhisha kutoka Asilimia 6.7 kwa mwaka 2011 hadi Asilimia 7.0 mwaka 2012.
Ameongeza kuwa hali hiyo inatoa matumaini makubwa hasa
ikizingatiwa kuwa ukuaji wa uchumi katika Bara la Afrika ni Asilimia
5.3 ambapo kwa upande wa Ukuaji wa uchumi wa Dunia ni Asilimia 2.9.
Kuhusu Zao la Karafuu Dkt. Shein amesema kuwa Shirika la
Biashara la Taifa ZSTC linatarajia kununua tani 4,016 kwa mwaka 2013 na
kuwaomba Wananchi waendelee kushirikiana na Serikali katika kupambana na watu
wanaofanya Magendo ya Karafuu.
Awali Akimkaribisha Rais Shein kutoa Hotuba yake Waziri wa
Katiba na Sheria Aboubakar Khamis Bakary alisema Serikali imepanga Sala na
Baraza la Idd katika Siku kuu zote za IDD-EL HAJJ zitakuwa zikifanywa kitaifa
katika Mikoa yote ya Unguja na Pemba ambapo kwa mara hii Swala ya Idd
ilifanyika kijiji cha Marumbi Mkoa wa Kusini Unguja.
alifahamisha kuwa Serikali imeamua kufanya hivyo ili Wananchi wa
Mikoa yote ya Unguja na Pemba wapate fursa ya kuswali pamoja na Viongozi wao
Wakuu wa Kiserikali lakini kwa upande wa Swala ya IDD EL-FITRI itaendelea
kuswaliwa kitaifa katika Mkoa wa Mjini Magharibi.
No comments:
Post a Comment