Header Ads

Baada ya Wanawake wa Saudi Arabia kusema wanaandamana leo ili waruhusiwe kuendesha magari

Ukraine ProtestLeo October 26 2013 ndio Wanawake nchini Saudi Arabia wamepanga kuandamana kupinga wao kunyimwa kuendesha magari sehemu yoyote nchini humo ikiwa ni nchi pekee duniani ambayo inakataza Wanawake kuendesha magari hata kama wanaweza.
saud arabia 7
Unaambiwa kwa sasa Mamlaka za Saudi Arabia zimewaonya Wanawake hao kutoandamana  katika maandamano hayo yatakayokua ya aina yake na ya tatu kutokea nchini humo toka mwaka 1990 ambapo Wanawake kadhaa walikamatwa na wengine kuachishwa kazi, onyo hilo linakwenda pia kwa Mwanamke yeyote ambae amepanga kuendesha gari
saudia 4

Msemaji wa Serikali amesema Mwanamke yoyote atakae endesha gari leo atachukuliwa hatua za kisheria ambapo wakati siku hii ya kuandamana ikisubiriwa Wanawake kadhaa wa Saud Arabia tayari walishaweka video zao wakiendesha magari sehemu mbalimbali za Saudia lakini mpaka sasa hawajakamatwa.
saud arabia 8
Mpaka sasa zaidi ya watu elfu 17 wamesain kura ya ndio itakayo waruhusu Wanawake wa Saudi kuendesha magari ambapo pia idadi ya Wanaume wanaosupport imeendelea kuongezeka kwa kasi.



No comments:

Powered by Blogger.