Header Ads

Airtel postpaid customer's now can pay their monthly bill via Airtel money.

Kulia ni Mkurugenzi wa kitengo cha  Airtel huduma kwa wateja Adriana  Lyamba akijaribu kulipia bili kupitia huduma mpya ya Airtel money mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya  uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money leo ambapo sasa inawawezesha  wateja wake wa huduma ya malipo ya baadaye kulipia bili zao za kila
mwezi kupitia huduma ya Airtel money popote walipo. Kushoto ni afisa  wa Airtel kitengo cha huduma ya malipo baadae akifuatilia uzinduzi huo leo.
 Kulia ni Mkurugenzi wa kitengo cha  Airtel huduma kwa wateja adriana  Lyamba akiongea na waandishi wa wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Money leo.ambapo sasa inawawezesha wateja wake wa  huduma ya malipo ya baadayekulipia bili zao za kila mwezi kupitia  huduma ya Airtel money popote  walipo. Kushoto ni afisa wa Airtel kitengo cha huduma ya malipo baadae   Pauline Shoo   akifuatilia uzinduzi huo leo.
 Afisa malipo ya huduma kwa wateja wa malipo baadae Bi Pauline  Shoo akielezea jinsi huduma hiyo inavyofanya kazi kupitia (Menu) au  Orodha ya huduma ya Airtel Money. huduma hii inawawezesha wateja wa  Airte  wa malipo ya baadaye  kulipia bili zao za kila mwezi kupitia huduma ya Airtel money popote  walipo.
 Kushoto ni Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Adrina Lyamba na  ofisa huduma kwa wateja wa malipo baadae bi Pauline Shoo wakiwa  wameshikilia vipeperushi vya huduma mpya inayowawezesha wateja wake wa huduma ya malipo ya baadaye kulipia bili zao za kila mwezi kupitia  huduma ya Airtel money popote walipo. Kushoto ni afisa wa Airtel kitengo cha huduma ya malipo baadae bi Pauline Shoo.
========  =======  =======
Wateja wa malipo ya mwezi (POSTPAID)  Airtel sasa kulipia Ankra zao
kupitia  huduma ya Airtel Money

Dar es Salaam 17, 2013 katika mwendelezo wa kutoa suluhisho na
kuboresha huduma za kifedha,  Airtel Tanzania sasa inawawezesha wateja
wake wa huduma ya malipo ya baadaye kulipia bill zao za kila mwezi
kupitia huduma ya Airtel money.

Akiongea juu ya huduma hii mpya, Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za
wateja wa baadaye bi Adriana Lyamba alisema "Airtel Leo tunayo furaha
kuwafahamisha wateja wetu wa malipo ya mwezi (postpaid) kuwa malipo ya
ankra zao za simu za kila mwenzi yamerahisishwa zaidi kwa kupitia
huduma ya Airtel money ambapo kwa sasa hakuna haja ya kwenda benki au
kwenye ofisi za Airtel kulipia bill zao,  wateja wote wanaweza kufanya
malipo kwa kupitia huduma ya Airtel money.

Tunao wateja wa mashirika ya binafsi , Umma, serikali, UN agencies,
NGO na mashirika madogo madogo SME  kutoka katika mikoa mbalimbali
nchini wanaotumia huduma zetu za  malipo ya mwisho wa mwenzi yaani
huduma ya Postpaid

Tumeanzisha huduma ya kulipia bill kwa kupitia Airtel money  ili
kuweza kukabili changamoto mbalimbali tulizokuwa nazo huku tukiongeza
mapato katika ukusanyaji wa madeni na kuwaondelea wateja wetu usumbufu wa kutembea umbali mrefu kufanya malipo na kutoa rahisi katika huduma zetu.

 Bi Adriana Lyamba alisema, Tunaamini huduma hii italeta ufanisi
mkubwa katika huduma zetu na kuongeza wigo mpana wa malipo ya anka
zao. Na nachukua fulsa hii kuwashukuru wateja wetu kwa kutumia huduma
zetu mbalimbali katika kuendesha shughuli za kibiashara, kiuchumi na
kijamii

Akiongea jinsi ya kulipia ankra za simu Afisa huduma za baada Bi
Pauline Shoo  alisema Kupata huduma hii ni rahisi , piga *150*60#  na
kuunganishwa na menu ya Airtel money, kisha bonyesha kulipia bill,
andika neno la biashara postpaid - malipo ya mwenzi, ingiza kiasi ,
number ya account yako ya post paid kisha bonyeza ok na mojakwamoja
utapa uthibitisho wa malipo yako.

huduma ya Airtel money yaani pesa mkononi ni huduma ya kifedha
inayotolewa na Airtel ikiwa na lengo la kurahisisha malipo ya anka
mbalimbali na kuwezesha upatikanaji wa pesa yaani  kutuma na kutoa
fedha kuwa rahisi na uhakika mahali popote nchini

kwa sasa Airtel kupitia promosheni yake ya hakatwi mtu hapa
inawawezesha wateja wake nchi nzima kutuma na kutoa pesa BURE bila
makato yoyote .

No comments:

Powered by Blogger.