Mtangazaji
wa Redio ya Clouds FM, Alex Lwambano akitofautisha rangi za bia kwa
kuangalia wakati wa mashindano ya kuonja ladha ya bia yaliyoandaliwa na
Ka mpuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Dar
es Salaam katika Makao Makuu ya TBL mwishoni mwa wiki. Walioibuka
washindi katika kinyang'anyiro hicho ni; Mpigapicha wa gazeti la
Tanzania Daima, Francis Dande (nafasi ya kwanza), Mpigapicha wa gazeti
la Mwananchi, Venance Nestori (nafasi ya pili) na Clifod Ndimbo wa Radio
Times FM aliyeambulia nafasi ya tatu.
Washindi
wa uonjaji wa ladha ya bia za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) wakiwa
katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa na kukabidhiwa zawadi zao
katika mashindano yaliyowashirikisha waandishi wa habari Mkoa wa Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki katika Makao Makuu ya TBL, Dar es Salaam.
Katikati ni Mshindi wa kwanza, Mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima,
Francis Dande, Kulia ni mshindi wa pili Venance Nestory Mpiga picha wa
gazeti la Mwananchi na Clifod Ndimbo wa Radio Times FM aliyeambulia
nafasi ya tatu.
Mwandishi
wa habari wa gazeti la The African, Sylvester Joseph akitofautisha
rangi za bia kwa kuangalia wakati wa mashindano ya kuonja ladha ya bia
yaliyoandaliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa waandishi wa habari
wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Makao Makuu ya TBL, mwishoni mwa wiki.
Meneja
Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi
(kushoto) akimkabidhi zawadi ya katoni mbili za bia, Mpigapicha wa
gazeti la Mwananchi, Venance Nestori aliyeshika nafasi ya pili katika
mashindano ya kuonja bia
Meneja
Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi
(kushoto) akimkabidhi zawadi ya katoni tatu za bia, Mpiga picha wa
gazeti la Tanzania Daima, Francis Dande ambaye aliibuka mshindi wa
kwanza wa mashindano ya kuonja bia yaliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa
waandishi wa habari wa mkoa wa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Venance Nestori (nafasi ya pili) na
Clifod Ndimbo wa Radio Times FM aliyeambulia nafasi ya tatu.
Mtaalamu
wa Upishi wa Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Deusdedith Maganga
(kushoto), akitoa maelezo kwa waandishi wa Mkoa wa Dar es Salaam, jinsi
unga wa mahindi unavyotumika kutengenezea bia walipotembelea kiwanda cha
bia cha TBL Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.
Baadhi
ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakipata maelezo kutoka
kwa Mtaalamu wa Upishi wa Bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
Deusdedith Maganga (kulia), kuhusu hatua mbalimbali za utengenezaji wa
bia walipotembelea kiwanda cha bia cha TBL Dar es Salaam, mwishoni mwa
wiki.
Meneja
Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi
(kushoto) akimkabidhi zawadi ya katoni moja ya bia, Mtangazaji wa Radio
Times FM, pigapicha wa gazeti la Mwananchi, Venance Nestori aliyeshika
nafasi ya pili katika mashindano ya kuonja bia yaliyoandaliwa na
kampuni hiyo kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Dar es Salaam mwishoni
mwa wiki.
Reviewed by
crispaseve
on
5:04 AM
Rating:
5
No comments:
Post a Comment