TIGO YAZIDI KUMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI WA PROMOSHENI YA ZAMU YAKO KUSHINDA
Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
Tigo yawazawadia washindi wa
promosheni ya “ZAMU YAKO KUSHINDA”
14 Februari, 2012, Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imewazawadia washindi
wanne, kila mmoja shilingi milioni nne, (Tsh. 4,000,000/-) kama washindi
wa kwanza wa kila siku ambao wamepatikana katika promosheni
inayoendelea ya “Zamu yako Kushinda.” Halikadhalika washindi wengine
nane wamezawadiwa kompyuta aina ya laptop za Samsung. Washindi wamepatikana katika kipindi cha siku 4.
“Tunapoelekea mwisho
wa promosheni hii tungependa tuwashukuru wateja wetu wote walioshiriki,”
alisema Alice Maro, Afisa Mahusiano wa Tigo. “Wale ambao hawaja shinda
wasikate tamaa bado wana nafasi ya kushinda zimebaki
siku 5 tu na promosheni yetu itafikia mwisho,” alisema.
Washindi wa Tsh. 4,000,000/- ni Willy Mtenga (Arusha); Pendo Leverian
(Kihonda-Morogoro); Magren Maleko (Mbezi Kimara) na Frank Geoffrey
(Mbezi Beach).
Washindi wa laptop ni
Asma Abdallah (Magomeni); Esther Cheyo (Tabata Segerea); Liberty Lyimo
(Tabata Segerea); Juma Omar Lukengele (Kimara Bonyokwa); Ameir Bakari
(Buguruni); Blake Ally Blake (Mwananyamala); Erick Chuma (Tanga) and
Rashid Gunde (Ilala Sharif Shamba).
Ili kushiriki mtumiaji wa Tigo anatakiwa
kutuma neno “TIGO” kwenda 15571. Gharama kwa kila ujumbe ni Tsh 450.
Washiriki wanatakiwa kujikusanyia pointi nyingi ili kujiwekea mazingira
mazuri ya kujishindia zawadi. Washiriki pia watazawadiwa zawadi za
kutuma ujumbe wa bure kutoka Tigo kwenda mitandao yote Tanzania.
Watumiaji wa mtandao wa
Tigo wenye umri chini ya miaka 18, hawaruhusiwi kushiriki. Promosheni
hii ni kwa ajili watumiaji wa Tigo watanzania.
Kuhusu
Tigo:
Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania,
ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu
ya hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya
MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za
mkononikwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengikiurahisi kwa
wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibukaAfrika
na Amerika ya Kusini.
Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa
mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji
.Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na
zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja
wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa
yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa taarifa zaidi tembelea:
www.tigo.co.tz
Imetolewa
na:
Alice
Maro • PR-Tigo • Simu 255 715 554501
No comments:
Post a Comment