OFISI
YA RAIS IKULU-UTAWALA BORA
TAARIFA
KWA UMMA
TAMKO
LA SERIKALI KUHUSU MPANGO WA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA
UWAZI (OPEN GOVERNMENT PARTNERSHIP - OGP)
Tanzania
imeridhia kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa
Uwazri (Open Government Partnership – OGP). Mpango huu ni juhudi
za kimatifa katika
kuhimiza uendeshaji wa Serikali kwa uwazi zaidi, ushirikishwaji mkubwa
wa
wananchi, kudhibiti rushwa katika jamii na kuimarisha utoaji wa huduma
bora.
Vigezo
vya nchi kuwa mwanachama wa Mapango huu ni pamoja na kuandaa Mpango Kazi
wa
Kitaifa (Country Action Plan) kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi
na
wananchi.
Kwa
kuanzia, uandaaji wa utekelezaji wa Mpango huo utahusisha vipaumbele
katika
sekta tatu za Afya, Elimu na Maji ili kuimarisha uwazi, uadilifu na
uwajibikaji
katika utoaji wa huduma.
Mpango
huu sasa unaboreshwa kwa kupokea maoni na ushauri kutoka kwa Wananchi na
Wadau
mbalimbali. Njia za kukusanya maoni pamoja na Tovuti ya Wananchi (www.wananchi.go.tz),
barua
kupitia Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu, S.L.P. 9120, Dar es Salaam,
ujumbe
bila malipo kupitia simu ya mkononi (SMS) namba 0658-999222, barua
pepe: ogp@ikulu.go.tz.
Mpango
Kazi wa OGP Tanzania unapatikana kwenye Tovuti ya Wananchi – www.wananchi.go.tz . Wananchi na
Wadau
wengine wanaimizwa kushiri kikamilifu
kutoa maoni yao katika kuboresha Mpango Kazi wa OGP Tanzania. Mwisho wa
kupokea
maoni/ushauri au mapendekezo ni tarehe 30/03/2012.
IMETOLEWA NA OFISI YA RAIS
IKULU – DAR ES SALAAM
TAREHE:.15 Februari 2012.
No comments:
Post a Comment