MNADA MPYA WA KITWIRU IRINGA WACHUKUA UMAARUFU MKUBWA
Mnada mpya wa Manispaa ya Iringa uliopo eneo la Kitwiru umezidi kujizolea umaarufu mkubwa kwa nyama choma na kuanza kuuzidi mnada wa Dodoma ambao umekuwa maarufu hapa nchini .
Tayari eneo hilo limejengwa vizuri na kuwekwa huduma zote za jamii kama choo ,jengo la kupumzika na huduma ya maji na idadi ya watu kutembelea mnada huo imezidi kuongezeka zaidi .
Zipo taarifa kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kuwa wafanyabiashara ndogo ndogo wa mnada wa Miyomboni jumapili ijayo watahamishiwa katika mnada huo ambao umejizolea umaarufu mkubwa . (Kwa hisani ya Blog ya Francis Godwin)
No comments:
Post a Comment