Mshindi wa Uchaguzi mdogo wa Jimbo la
Uzini, kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mohammed Raza, akiwaonesha
waandishi na wananchi cheti cha kuthibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi
huo.
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kati,
Mussa Ali Juma, akimkabidhi hati ya ushindi Mshindi wa Uchaguzi Mdogo
wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza, baada ya kutangazwa matokeo.
Wagombea wakifuatilia matokea
ya kura yakisomwa na Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya Kati Unguja, katika
Ukumbi wa Ofisi ya Wilaya ya Dunga.
Msimamizi wa Uchaguzi Wilaya ya
Kati Mussa Ali Juma, akitowa matokeo ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Uzini, baada ya kumaliza zoezi la kuhesabu kura katika ukumbi maalum
ulioandaliwa na kuwajumuisha Wagombea na Wananchi mbalimbali.
Mgombea wa CHADEMA Ali Mbarouk
Mshimba, akitowa shukrani kwa Wananchi waliompigia kura, baada ya
kutangazwa mshindi katika ukumbi wa Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya
Kati Dunga.
No comments:
Post a Comment