Header Ads

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stellah Manyanya (kulia), akimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro,baada ya mwenge huo kumaliza mbio zake mkoani Rukwa, katika hafla iliyofanyika jana, kijiji cha Mkutano wilayani Mbozi.
Askari wa kutuliza ghasia na skauti wakiulinda mwenge wa uhuru baada ya kuwasili viwanja vya Bomani wilayani Mbozi.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa,Mtumwa Rashid Halfan, kutoka kaskazini Unguja, akivuta pazia kuashiria uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa Kiume wa Sekondari ya Mwalimu Jk.Nyerere iliyopo Tunduma wilayani Mbozi mkoani Mbeya.
Wakimbiza Mwenge kitaifa wakisikiliza wimbo wa kupinga Rushwa uliokuwa ukiimbwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ihanda iliyopo Mozi wakati wa uzinduzi wa klabu ya wapinga rushwa shuleni hapo.
Wananchi wa Mkoa wa Mbeya wakishangilia baada ya mwenge wa uhuru kuwasili katika kijiji cha mkutano ambacho kipo mpakani mwa mkoa wa Rukwa na Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Gabriel Kimolo (kulia), akimkabidhi mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini,Evance Balama, baada ya mwenge huo kumaliza mbio zake wil;ayani Mbozi.Makabidhiano hayo yalifanyika Songwe Viwandani mkoani Mbeya.Mwenge huo mkaoni Mbeya utafungua miradi yenye thamani ya sh.bilioni 2.6 na Wilayani Mbozi umefungua miradi mitatu ya sh.milioni 156. (PICHA ZOTE NA DOTTO MWAIBALE)

No comments:

Powered by Blogger.