Header Ads

Wanachadema wakiwa nje ya mahakama leo mchana kusikiliza shauri la mbunge wao.Habari tulizopata sasa hivi toka kwa Henry Kilewo(katibu wa BAVICHA Kinondoni) ambaye yuko Arusha zinasema kuwa mamia ya watu wamekusanyika na kubaki viwanja vya NMC wakidai hawatatoka hapo hadi mbunge wao aachiliwe huru. Mwenyekiti wa Chadema,Mh Mbowe, Dkt.Slaa na Tundu Lisu wapo pia usiku huu.Inasemekana Kamishna Chagonja anaongea na Lisu sasa hivi kuona kama watu wanaweza kutawanyika. Picha/Habari Kwa Hisani ya Mjengwablog

No comments:

Powered by Blogger.