WANAFUNZI UDOM WAPATA KIWEWE BAADA YA BODI YA MIKOPO KUTOA MAJINA YALIYO NA KASORO NA MWISHO WA KUSAJILI UPYA NI LEO
Baadhi ya Wanafunzi Wa UDOM wakirudia
kujisajili huku wengine wakiangalia majina yao kwenye tovuta ya bodi ya
mikopo kuona kama majina yao ya makosa.Wale ambao majina yao ya kasoro
wametakiwa kujaza tena na kutuma upya huku ikiwa mwisho ni leo na baadhi
ya majina yakiwa hayajatoka.
Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma
(UDOM) wakiwa bize sana kujisajili kusajili masomo yao ya muhula wa
kwanza kupitia mtandao wa intaneti na wengine wakirudia kujisajili tena
kupitia intaneti kwaajili ya kupewa mkopo baada ya majina yao kurudishwa
yakiwa na kasoro .Wanafunzi Hao wakionekana kuchoka kutokana na kasi ya
intaneti kuwa chini na kuleta usumbufu
Kama
Wanavyooneka wanafunzi wakiwa bize kusajili masomo yao huku wengine
wakiangalia majina yaliyotolewa ya wanafunzi ambao majina yao yana
kasoro na kutakiwa kurudia kujazwa upya na kutumwa tena kupitia mtandao
wa kompyuta huku mwisho wa kufanya hivyo ni leo tarehe 26/10/2011 wakati
kuna majina mengine yanaendelea kutolewa na bodi ya mikopo kupitia
tovuti yao.
No comments:
Post a Comment